
Mwenye picha hapo juu ni Binti wa Kitanzania anaitwa Vivian Mhagama Mvungi. Alizaliwa Dar es Salaam Mwaka 1999.
Aliwahi kuishi Mlandizi na Morogoro na wazazi wake, Mama yake anaitwa Irene, Baba yake anaitwa Hussen Mvungi na Mdogo Wake anaitwa Abdulrahman.
Vivian alikwenda Lubumbashi , Kongo mwaka 2009 akiambatana na Mama yake mzazi.
Mama yake mzazi alimtelekeza na kumuacha akilelewa na Padri wa kanisa la Orthodox katika kitongoji cha Luashi . Kwasasa ameolewa na ana watoto wawili. Anataka kuwaona na kuwasiliana na wazazi wake au ndugu zake waliopo Tanzania. Kwa taarifa zozote kuhusu suala hili tafadhali wasiliana na Ofisi ya Ubalozi Mdogo wa Tanzania Lubumbashi kupitia namba za simu +243970766605 au +255787220162.
No comments:
Post a Comment