TANZANIA tuna Kila sababu ya kushukuru kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika (Mission 300 AFRICA ENERGY SUMMIT) unaofanyika January 27-28/2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere JNICC Dar es salaam.
Mkutano huu umekuja wakati muafaka ambao Tanzania imepiga hatua kubwa katika Suala Zima la Upatikanaji Wa Suala Zima la nishati.
Hii imechangiwa na Uongozi thabiti wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan ambae amekuwa kinara wa masuala haya.
Ni Rais ambae ametekeleza kwa vitendo azma yake ya Kuona jitiada kubwa inawekwa kwenye Uzalishaji na usambazaji wa umeme.
Waswahili husema UKIONA KIVULI KIMENYOOKA BASI NA MTI UTAKUWA UMENYOOKA, Hapa tunazungumzia namna Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) na wakala wa umeme Vijijini (REA) kwa pamoja wameishi maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha Nchi inatoka kwenye Giza kupitia Kasi ya usambazaji umeme Vijijini.
Licha ya kuwa na vyanzo mbalimbali vya nishati, Kwa Sasa Tanzania inajivunia kukamilisha kwa Asilimia 99.6 Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere JNHPP, Bwawa la nne kwa ukubwa Afrika lenye uwezo wa kuzalisha Megawatt 2,115.
Bwawa hili linawezesha Nchi kuwa na Umeme wa kutosheleza Matumizi ya Ndani na pia kuuza umeme kwa Nchi jirani.
Hata Ile kero ya kukatikakatika kwa umeme au mgao Sasa imebaki historia, Wananchi wanafurahia Upatikanaji Wa umeme wa uhakika, hata Upande wa Viwanda kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la wawekezaji nchini.
Sio Umeme pekee, Tanzania pia imepiga hatua kubwa katika Suala Zima la Matumizi ya Nishati safi ya kupikia hususani matumizi ya Gas.
Hapa tumeshuhudia mwamko mkubwa wa Wananchi kuanza kutumia nishati ya Gas kupikia majumbani na Maeneo ya biashara.
Tumeshuhudia familia nyingi zikiachana na Matumizi ya Kuni ambayo yalikuwa chanzo Cha uharibifu wa mazingira na pia kuathiri Afya za kinamama.
Kama Nchi tumejipanga, tumejidhatiti na tutazidi kusimamia Ajenda ya kupeleka umeme kwa wananchi milioni 300 barani Afrika ifikapo 2030 kati ya watu milioni 685 ambao bado hawana umeme.
Nasi kama Tanzania tunasema MABADILIKO ENDELEVU YA SEKTA YA NISHATI NI MUHIMU KWA MAENDELEO YA AFRIKA.
No comments:
Post a Comment