Na Mwandishi wetu
Mashindano
ya Samia Supa Cup ya Kata ya Msasani yameanza kwa vishindo huku huku
Diwani wa Kata hiyo, Luca Neghest akimwaga vifaa vya michezo kwa timu
mbalimbali.
Mashindano hayo yalizinduliwa na mwenyekiti wa Chama
Cha Mapinduzi Manispaa ya Kinondoni, Shaweji Abdalla Mkumbula kwa
kushirikiana na viongozi wengine mbalimbali pamoja na Katibu Mwenezi wa
CCM Dar es Salaam, Ally Bananga, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Msasani,
Nyerere Mnyupe na Diwani Kata ya Tandale,Abdallah “Chief” Saidi.
Uzinduzi
huo ulipambwa na maandamano maalum yaliyowashirikisha wakazi
mbalimbali, pikipiki aina ya bajaj ambayo yaliongozwa na Diwani Neghest.
Mkumbula
alisema kuwa mashindano ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Samia
Suluhu Hassan za kuendeleza michezo nchini ambapo mpaka sasa Tanzania
imefikia viwango vya juu kabisa.
Alisema kuwa kila mwanamichezo
anajua jinsi gani Rais Samia alivyochangia maendeleo ya michezo mpaka
sasa na kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi nyota zinazotamba
katika michezo barani Afrika.
“Kwa timu yetu ya Taifa, Taifa
Stars, kwa sasa tumefanikiwa kuingia mara mbili fainali za Afcon na
mwaka 2027, sisi tutakuwa mwenyeji. Sisi kama wasaidizi wake, ni jukumu
kumsaidia kwa kupitia Ilani ya CCM.
Nampongeza Diwani Luca
Neghest kwa kuandaa mashindano haya kwa kushirikisha soka, rede, bao na
drafti kwa Kata ya Msasani,” alisema Mkumbula.
Kwa upande wake,
Katibu Mwenezi wa Dar es Salaam, Ally Bananga alimpongeza Diwani Neghest
kwa kuendelea kutimiza ilani ya CCM na kuwaomba wakazi wa Kata hiyo
kuendelea kumpa sapoti katika juhudi hizo.
Bananga alisema kuwa
Diwani Neghest ameunga mkono juhudi za Rais Samia kwa kuandaa mashindano
hayo yenye hamasa ya hali ya juu na tija kwa taifa.
“Kila mtu
anajua kwa Rais Samia amesapoti Ndondo Cup, wachezaji wengi wa Tanzania
wanatokea huku kwenye mashindano kama haya kwani yanaibua vipaji. Wito
wangu kwa wadau ni kumpa sapoti kubwa Diwani Neghest na kuboresha vwanja
vya michezo ikiwa pamoja na huu wa Msasani,” alisema Bananga.
Naye,
Mwenyekiti wa CCM wa Msasani, Nyerere Mnyupe aliwapongeza wanamichezo
mbalimbali waliojitokeza kuunga mkono juhudi za Diwani Neghest za
kutelekeza ilani ya CCM kwa kuandaa mashindano ya aina mbalimbali yenye
tija huku Diwani Kata ya Tandale,Abdallah Saidi akisema atatumia
mashindano hayo kusaka vipaji kwa ajili ya timu ya KMC.
Kwa
upande wake, Diwani Neghest alisema kuwa amefurahishwa na idadi na
hamasa kubwa ya wakazi wa kata ya Msasani na sehemu nyingine kushiriki
katika uzinduzi rasmi wa mashindanohayo.
“Nimeruhai sana kuona
lengo la kuunga mkono juhudi za kuendeleza michezo kupitia ilani ya CCM
kutimia. Idadi ya watu na hamasa imenipa faraja sana. Nawashukuru
viongzi wa CCM mliofika kunipa sapoti katika tukio hili kenye kutimiza
ilani ya chama chetu kwa agizo la Rais Samia,” alisema Neghest.
Diwani
Neghest alisema kuwa bingwa wa mashindano hayo atazawadiwa fedha
taslimu, Sh4 million ambapo mbali ya soka, pia kiasi kama hicho cha
fedha watazawadiwa washindi wa rede kwa wanawake na washindi wa pili
watazawadiwa Sh 2 milioni kila mmoja.
Neghest alisema kuwa
mshindi wa kwanza kwa mchezo wa drafti atazawadiwa sh 2 milioni wakati
mshindi wa pili atazawadiwa Sh milioni moja. Kwa upande wa bao, Neghesti
alisema kuwa mshindi atapata Sh 1 milioni na mshindi wa pili
atazawadisha Sh500, 000. Katika uzinduzi huo, timu ya Juventus FC
iliifunga Don Bosco mabao 2-1.
3.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa Manispaa ya Kinondoni, Shaweji
Abdallah Mkumbula akigawa vifaa mwakilishi wa timu za rede
zitakazoshiriki katika mashindano ya Samia Supa Cup Msasani
yaliyoandaliwa na Diwani Luca Neghest.
Msafara wa pikipiki aina za Bajaj ukipamba uzinduzi wa mashindano ya Samia Supa Cup Msasani yaliyoandaliwa Diwani Luca Neghest.
4.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa Manispaa ya Kinondoni, Shaweji
Abdallah Mkumbula akigawa vifaa mwakilishi wa timu za drafti timu
zitakazoshiriki katika mashindano ya Samia Supa Cup Msasani
yaliyoandaliwa na Diwani Luca Neghest.
Mashabiki
wa soka wakifuatilia mechi ya uzinduzi kati ya Juventus FC na Don Bosco
ya mashindano ya Samia Supa Cup Msasani yaliyaondaliwa na Diwani Luca
Neghest. Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Jackson Msilombo,
Juventus FC ilishinda kwa mabao 2-1.
Wawakilishi
mchez wa rede wakiwa na vifaa vilivyokabidhiwa kwao na mwenyekiti wa
CCM Manispaa ya Kinondoni Sheweji Abdallah Mkumbula kwa niaba ya Diwani
wa Msasani, Luca Neghest kwa ajili ya kutumika katika mashindano ya
Samia Supa Cup Msasani.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi wa Manispaa ya Kinondoni, Shaweji Abdallah
Mkumbula akizungumza kabla ya mechi ya ufunguzi wa mashindano ya Samia
Supa Cup Msasani kati ya timu ya Don Bosco na Juventus kwenye uwanja wa
Msasani jijini. Mashindano hayo yameandaliwa na Diwani Luca Neghest.
Diwani
wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Msasani Luca Neghest (mwenye miwani)
akishiriki katika maandamano wakati wa uzinduzi wa Samia Supa Cup
Msasani aliyoyaandaa.
No comments:
Post a Comment