Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo amesema kuwa ulipaji wa kodi ndio maendeleo ya Taifa lolote duniani.
Kayombo aliysema hayo katika mkutano na Wafanyabiashara wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma uliofanyika katika ukumbi wa FDC.

Ameaema sambamba na kuwashukuru Wafanyabiashara pia amewataka kuendelea na tabia hiyo ya ulipaji wa kodi.
Kayombo amekata keki na kuwalisha viongozi wa wafanyabiashara na wafanyabiashara wengine.
Pia amewahamasisha Wafanyabiashara wa Mkoa wa Ruvuma walipe kodi zao za awamu ya nne mapema kabla ya tarehe 31/12/2024.
No comments:
Post a Comment