Na Mwandishi Wetu
MWANAMITINDO
wa Kimataifa Millen Happiness Magese amekabidhi kitita cha Sh.milioni
tatu kwa Mwanamitindo Elizabeth Masuka aliyeibuka mshindi wa Samia
Fashion Festival Zanzibar mwaka 2024.
Millen Happiness Magese
aliyekuwa Jaji Mkuu wa Samia Fashion Festival Zanzibar alikabidhi hundi
ya fedha yenye thamani ya Sh.milioni tatu katika Hoteli ya Urban by City
Blue iliyopo Jijini Dar es Salaam ambapo alimuandalia chakula cha usiku
mwanamitindo huyo na fedha hizo zimetoka Kampuni ya Millen PRIVE $ Co
kupitia Millen PRIVE Lifestyle ambayo yeye ndio Mkurugenzi Mkuu.
Taarifa
ya Mwanamitindo huyo Mtanzania anayeishi nchini Marekani aliyoitoa kwa
vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam amesema kuwa katika tamasha la
Samia Fashion Festival Zanzibar yeye alikuwa Jaji Mkuu hivyo pamoja na
kutangaza washindi wa tamasha hilo, aliona umuhimu wa kuitambua kazi
kubwa iliyofanywa na wanamitindo walishiriki usiku huo na kumtangaza
Elizabeth Masuka kuwa Mwanamitindo bora wa tamasha hilo.
“Tunafahamu
kulikuwa na Samia Fashion Festival Zanzibar ambalo liliandaliwa na dada
yangu Khadija Mwanamboka na katika tukio hilo nilikuwa Jaji Mkuu ,hivyo
baada ya kutangaza washindi niliona umuhimu wa kuitambua kazi kubwa
iliyofanywa na wanamitindo walishiriki usiku huo na kumtangaza Elizabeth
Masuka kuwa Mwanamitindo bora wa Samia Fashion Festival Zanzibar mwaka
2024.
“Nimetoa fedha hizo Sh.milion tatu kwanza kwa kutambua
mchango wa wanamitindo wote ambao wamefanya kazi kubwa na nzuri wakati
wa tamasha hilo lakini fedha hizo ni katika kuwatia moyo wanamitindo
wanaochipukia katika medani za Wanamitido na tatu nimetoa fedha hizo
Sh.milioni tatu kwa Elizabeth Masuka kwa kutambua yeye ndio Mwanamitindo
bora wa Samia Fashion Festival Zanzibar mwaka 2024.,amesisitiza Millen
Happiness Magese.
Ameongeza kuwa amefurahishwa kufanyika kwa
Samia Fashion Festival Zanzibar kwani limethibitisha nafasi na umuhimu
wa wanamitindo nchini Tanzania lakini pia kutoa nafasi ya vijana wa
Kitanzania kuonesha uwezo wao katika kutawala Jukwaa la wanamitindo.
Ametumia
nafasi hiyo kukumbusha kuwa ni heshima kubwa kwake kuwa Jaji Mkuu wa
Samia wa Fashion Festival na anajivunia kushuhudia wanamitindo wote
walioshiriki na kuonesha uwezo wao huku akisisitiza kwa zaidi ya miaka
ishirini amejitolea maisha yake katika sekta ya mitindo, urembo.
Amefafanua
ameona jinsi mitindo inavyothaminiwa katika nchi za Ulaya na mataifa
mengine, si tu kama sanaa bali kama alama ya utambulisho, urithi, na
fahari.Ametoa rai kwa Watanzania kuunga mkono juhudi zinazofanywa na
wadau pamoja na Serikali chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan katika
kuinua na kuendeleza sekta ya utamaduni,mitindo na urembo.
Kwa
upande wake mwanamitindo Elizabeth amesema kukutana kwa mara ya kwanza
na Millen ilikuwa ni ndoto iliyotimia na amefurahi kumuona ana kwa ana
na kwa jinsi alivyo na mafanikio.
“Nimejifuza kitu kipya kutoka
kwake, zawadi ambayo alinipa ilikuwa furaha yangu ya pili baada ya kazi
nzuri ambayo imefanyika, namshuru sana na kumuombea Mungu aendelee
kumuweka kwa ajili yetu, ni mtu mwema sana, kutoka kwake niliona mtu
ambaye anataka kuona wanamitindo wengine nchini Tanzania wakifanikiwa.”
Mwanamitindo wa Kimataifa Millen Happiness Magese (kushoto) akimkabidhi hundi ya Sh.milioni tatu Mwanamitindo bora wa Samia Fashion Festival Zanzibar mwaka 2024 Elizabeth Masuka.Hafla ya kukabidhi hundi hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Urban by City Blue iliyopo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment