NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
WANAHARAKATI
wa Jinsia na Maendeleo wameiomba Serikali kuingilia kati na kutatua
changamoto zinazowakabili wanawake katika sekta ya afya, uchumi, na
uongozi ikiwemo ukandamizaji wa haki kwa mwanamke.
Akizungumza
leo,Novemba 13,2024 katika ofisi za Mtandao wa jinsia TGNP Mabibo-Jijini
Dar es Salaam, Mwanaharakati wa jinsia na Maendeleo, Sharifa Hassan
ameiomba serikali kudhibiti mianya ya Rushwa katika sekta ya afya ili
kutimiza dhamira yake ya huduma bure kwa mama mjamzito na mtoto.
"Ukienda
kujifungua unaambiwa ununue vifaa na hata kama vifaa ulibeba wanaacha
vifaa vyako wanatumia vifaa vyao ilimradi tu utoe fedha"Amesema.
Amesema
kumekuwa na huduma ambazo haziridhishi katika vituo vya kutoa huduma za
afya katika maeneo mbalimbali huku wengi wakihitaji fedha ndo waweze
kutoa huduma, jambo ambalo linakatisha tamaa
Aidha katika upande
wa biashara amesisitiza serikali kulivalia njuga suala la mgawanyo wa
meza kwani idadi ya wanaume wanaomiliki meza masokoni ni kubwa kuliko
wanawake Jambo ambalo linahafisha juhudi za mwanamke katika kujiimarisha
kiuchumi ambapo wanawake wengi wanapanga vitu vyao chini kwasababu ya
kuukosa meza.
Pamoja na hayo Sharifa ameshauri kwamba ili kuwa na
usawa katika uongozi inatakiwa kuundwe utaratibu ambao utasaidia uteuzi
wa moja kwa moja kwa uwakilishi wa mwanamke katika uongozi kwa sababu
wanawake wengi wanakwama kutokana na changamoto ya kiuchumi pamoja na
Rushwa ya ngono.
Naye Mwanaharakati Mussa Abdallah ameeleza namna
ambavyo mila kandamizi zinamnyima mwanamke nafasi ya kuimarika kiuchumi
na kujikuta akifanya kazi nyingi kwa wakati mmoja kwa kipato hafifu.
Wednesday, November 13, 2024
Home
Unlabelled
WANAHARAKATI WALIA NA UKANDAMIZAJI WA HAKI YA MWANAMKE KWENYE SEKTA YA AFYA, UCHUMI NA UONGOZI
WANAHARAKATI WALIA NA UKANDAMIZAJI WA HAKI YA MWANAMKE KWENYE SEKTA YA AFYA, UCHUMI NA UONGOZI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment