Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) imetoa mafunzo ya uchambuzi wa masuala ya kijnsia na bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa maafisa mipango/ bajeti, wachumi na maafisa maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii toka wilaya kumi na mbili katika mikoa ya Shinyanga, Mbeya, Morogro, Dodoma, Kilimanjaro, Mtwara, Iringa, Manyara na Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo Mtafiti na Mchambuzi kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Zainabu Mmari aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Lilian Liundi amesema lengo ni kuongeza uelewa juu ya umuhimu wa upangaji wa bajeti, mipango na sera zinazozingatia jinsia, miongoni mwa watoa maamuzi pamoja na kutambua mapengo yaliyopo kwenye eneo la ushawishi na kujenga uwezo wa stadi za utetezi kwa siku za usoni.
Amesema ni muhimu kuimarisha ujuzi wa watoa maamuzi wa ndani katika kutekeleza sera na programu zinazozingatia jinsia, ikiwa ni pamoja na kufanya uchambuzi wa kijinsia, kuweka shabaha zinazozingatia jinsia, na ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo pamoja na kutambua somo lililopatikana, changamoto na mafanikio ya shughuli zilizotekelezwa.
Mmari amesema makundi yanayoshiriki wanaamini wako sehemu ya kufanya maamuzi ya kuhakikisha bajeti inayotoka katika maeneo yao ikizingaatia jinsia kutokana na uchambuzi mbalimbali unaofanywa katika Manispaa ,Miji pamoja na Halmashauri na wakati mwingie ngazi za vijiji.
Mtafiti na Mchambuzi kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Zainabu Mmari aliyemwakilisha
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) Lilian Liundi akifungua mafunzo ya uchambuzi wa masuala ya kijnsia na bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa maafisa mipango/bajeti, wachumi na maafisa maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii toka wilaya kumi na mbili katika mikoa ya Shinyanga, Mbeya, Morogro, Dodoma, Kilimanjaro, Mtwara, Iringa, Manyara na Dar es Salaam.
Mwanaharakati wa masuala ya kijinsia na Uchumi kutoka TGNP Rebecca Mjema Kisenha akiwasilisha mada kwa maafisa mipango/bajeti, wachumi na maafisa maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii toka wilaya kumi na mbili katika mikoa ya Shinyanga, Mbeya, Morogro, Dodoma, Kilimanjaro, Mtwara, Iringa, Manyara na Dar es Salaam.
Baadhi ya maafisa mipango/bajeti, wachumi na maafisa maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii wakifuatilia mada wakati wa mafunzo ya uchambuzi wa masuala ya kijnsia na bajeti yenye mrengo wa kijinsia yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment