Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imeshiriki katika mkutano wa kwanza wa watumiaji wa Ndege nyuki za DJI uliofanyika katika ukumbi wa Millenium towers, leo tarehe 28 Novemba 2024.
Akifungua mkutano huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw. Daniel Malanga Mkurugenzi Udhibiti Uchumi kutoka TCAA amesema teknolojia ya Ndege nyuki inakuwa kwa kasi na kuleta mabadiliko katika sekta ya Anga na kwingineko na inakadiriwa kuzidi dola billioni 101 ifikapo Mwaka 2032.
Bw. Malanga amesema mabadiliko hayo yatachochea ukuaji wa kiuchumi na kwa kulitambua hilo Mamlaka imejizatiti kuhakikisha ulinzi, usalama na udhibiti mzuri wa teknolojia hizo.
Katika majadiliano ya Jopo yenye mada ya “Kubadilisha Tanzania kwa Teknolojia ya Ndege Nyuki”, Mkaguzi wa Ndege Nyuki kutoka TCAA Bw. Ibrahim Abdallah amesema kumekuwa na maendeleo makubwa katika teknolojia ya Ndege nyuki na kwa sasa hazitumiki tu katika kuchukua picha na video bali pia katika kilimo, uchimbaji wa madini, ramani na uchunguzi lakini pia katika utunzaji na ulinzi wa wanyamapori.
Mkutano huo umeandaliwa na Kampuni ya Techno Environment Investment ambao ni waratibu wa shughuli za DJI hapa Tanzania.
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi katika Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Daniel Malanga akiyemwakilisha Murugenzi Mkuu wa TCAA akizungumza wakati wa mkutano wa kwanza wa watumiaji wa Ndege nyuki za DJI uliofanyika katika ukumbi wa Millenium towers, leo tarehe 28 Novemba 2024.
Mkurugenzi wa Watumiaji wa Ndege nyuki za DJI, Ephraim Danford akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa watumiaji wa Ndege nyuki za DJI uliofanyika katika ukumbi wa Millenium towers, leo tarehe 28 Novemba 2024.
Baadhi ya wadau mbalimbali ambao ni watumiaji wa Ndege nyuki za DJI wakifuatilia hotuba kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi katika Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Daniel Malanga aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi ya ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa watumiaji wa Ndege nyuki za DJI.
No comments:
Post a Comment