HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 18, 2024

SERIKALI YAIPONGEZA TAASISI YA HAYDOM KWA KUTOA HUDUMA BORA ZA AFYA

 

Na Mwandishi Wetu, MANYARA

 

Serikali  imepongeza Taasisi ya Mafunzo ya Sayansi za afya Haydom kwa utoaji huduma  za afya ikiwa ni jitihada za kuunga Mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuwapatia huduma bora za afya wananchi.

 

Hayo yamesemwa mbele ya waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mbulu tarehe 17 Novemba 2024 na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Mizengo Pinda (Mb.) akimwakilisha Waziri wa Fedha. Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba kwenye Sherehe ya Maadhimisho ya Miaka 40 ya Taasisi hiyo iliyopo Wilayani Mbulu Mkoani Manyara.

 

"Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imatambua mchango wa kanisa katika kuunga mkono juhudi za serikali za kuwapatia wananchi huduma bora" amesema Mhe. Pinda 

 

Mhe. Pinda amewaasa wanafunzi wa Taasisi hiyo kutumia vema elimu wanayoipokea kwa  kuendelea kujifunza kwa moyo wa kujitoa ili kuongeza ubunifu na kuondoa changamoto zinazoikabili sekta ya Afya hapa nchini.

 

"Nawaasa wanafunzi na wahitimu wa Taasisi hii Kuendelea kuwa na ari ya kujifunza, ubunifu na kujitolea katika Kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya afya" amesema Mhe. Pinda 

 

Naye Msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Mbulu John Nade ameishukuru Serikali ya awamu wa sita kwa kuiongezea taasisi hiyo nafasi za udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa Masomo 2024/25 na 2025/26

 

"Tunaishukuru sana Serikali ya Jamhuri Muungano wa Tanzania kupitia ofisi ya rais Tamisemi kwa uamuzi wake wa kuipa taasisi hii wanafunzi 60 kwa mwako 24/25 na Wanafunzi 40 kwa mwaka 2025/26 kwa fani ya Radiolojia" ameseme John Nade Msaidizi wa Askofu.

 

Kwa Upande Wake Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mhe. Fratei Gregory Massay amepongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kupeleka watumishi wa kutoa huduma katika Taaasisi Hiyo.

 

"Niishukuru Serikali hasa Rais wetu wa Tanzania Mama yetu Dkt. Samia Suluhu hassan ameshatusaidia watumishi watano mpaka sasa na sio hapa tu hata hosptali yetu pia ametuletea" amesema Mhe. Fratei Mbunge wa Jimbo mbulu Vijijini.

 

Taasisi ya Mafunzo ya Sayansi za afya Haydom ilianzishwa kwa lengo la kusaidia kujenga uwezo wa kitaaluma na kutoa mafunzo bora katika nyanja mbalimbali za Sayansi za afya na kuchangia kuboresha huduma za afya ndani na nje ya nchi.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza wakati wa Sherehe ya Maadhimisho ya Miaka 40 ya Taasisi ya Mafunzo ya Sayansi za afya Haydom iliyopo Wilayani Mbulu Mkoani Manyara tarehe 17 Novemba 2024
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akisisitiza jambo wakati akikakgua huduma za afya zinazotolewa na Taasisi ya Mafunzo ya Sayansi za afya Haydom tarehe 17 Novemba 2024 Mkoani Manyara.

Sehemu ya waumini wa kanisa la KKKT wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda (hayuko pichani) wakati wa maadhimisho ya miaka 40 ya Taasisi ya Mafunzo ya Sayansi za afya Haydom yaliyofanyika Wilayani Mbulu Mkoani Manyara tarehe 17 Novemba 2024.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad