HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 27, 2024

RAIS MSTAAFU DK. KIKWETE ASHIRIKI KATIKA ZOEZI LA UPIGAJI KURA KUCHAGUA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA KIJIJINI KWAKE MSOGA

 Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika foleni tayari kushiriki katika zoezi la upigaji kura wa viongozi wa serikali za mitaa kijijini kwake Msoga, wilaya ya Bagamoyo jimbo la Chalinze, mkoa wa Pwani. Mwenye shati la kijani ni Mbunge wa Chalinze na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe Ridhiwani Kikwete ambaye pia amepiga kura kwenye kituo hicho.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika zoezi la upigaji kura wa viongozi wa serikali za mitaa kijijini kwake Msoga, wilaya ya Bagamoyo jimbo la Chalinze, mkoa wa Pwani leo asubuhi.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mdogo wake Mohamed Kikwete (kulia kwake) na Mbunge wa Chalinze na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe Ridhiwani Kikwete na mwanakijiji mwenzao akiwa katika nyumba ya babu yake aliyokulia baada ya kushiriki katika zoezi la upigaji kura wa viongozi wa serikali za mitaa kijijini kwake Msoga, wilaya ya Bagamoyo jimbo la Chalinze, mkoa wa Pwani leo asubuhi.
Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wanahabari baada ya kushiriki katika zoezi la upigaji kura wa viongozi wa serikali za mitaa kijijini kwake Msoga, wilaya ya Bagamoyo jimbo la Chalinze, mkoa wa Pwani leo asubuhi.

PICHA NA ISSA MICHUZI

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad