WATAALAMU wa ununuzi na Ugavi hapa nchini wametakiwa kuwa wazalendo na kuzingatia maadili, weledi, kanuni na taratibu katika kutekeleza majuumu yao ili kuepuka kuzalisha hoja za Ukaguzi zinazopelekea halmashauri kupata hati chafu ikiwemo kuzingatia vipengele vya mikataba ambavyo Serikali inaingia kutokana na Ununuzi kwenye miradi mbalimbali nchini.
Hayo yamesemwa leo mkoani Arusha na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Missaile Musa wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi kutoka Taasisi na Halmashauri mbalimbali zilizopo katika Mkoa wa Arusha.
Musa amewataka wataalam hao kujiepusha na vitendo vya rushwa na kujikita zaidi katika kusimamia kikamilifu fedha zote za umma zinazotengwa kwa ajili ya miradi mbalimbali kufikia malengo waliyojiwekea kama mkoa.
“Lakini pia weledi na maadili ni msingi mkubwa katika kuhakikikisha miradi inatekelezwa ikiwa na viwano bora hivyo lazima eneo la Ununuzi lingaliwe vizuri na ikibainika kuna ukiukwaji wa sheria wahusika watachukuliwa hatua za kinidhamu,”
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Godfred Mbanyi amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wataalamu hao juu ya sheria mpya ya ununuzi na namna ya kusimamia mikataba.
Mbanyi amesema hivi karibuni Bodi hiyo ilifanya ukaguzi kwenye maeneo mbalimbali na kubaini kunabaadhi ya maofisa Ununuzi na Ugavi hawasajiliwa na Bodi hiyona kusisitiza ni vema wakafuata sheria ili wasije kumbana na adhabu.
Amesema kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo katika maeneo mengi hapa nchini ni wataalamu wa ununuzi kufanya kazi pasipo kusajiliwa na Bodi hiyo jambo ambalo ni kinyume cha sheria na kuwataka wale wote ambao hawajasajiliwa wajisajili mara moja.
“Natoa wito kuzingatia sheria kanuni na taratibu za Ununuzi katika kutekeleza majukumu yenu,na nawataka wale wote ambao hawajasajiliwa na Bodi kujisajili haraka iwezekanavyo kwani iko kwa mujibu wa sheria na anayefanya kazi bila kusajiliwa anavunja sheria za nchi”amesema Mbanyi
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Missaile Musa akizungumza kuhusu maadili kwenye taaluma ya ununuzi na ugavi wakati wa kufungua mafunzo ya siku mbili kwa Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi kutoka taasisi na Halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji (PSPTB), Bw. Godfred Mbanyi akitoa maelezo kuhusu kazi za bodi pamoja na lengo la mkutano Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi kutoka Taasisi na Halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Arusha wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, John Kayombo akizungumza namna wanavyoshirikiana na maafisa ununuzi ili kuweza kusimamia maadili ya kazi zao wakati wa wakati wa ufunguzi mafunzo ya siku mbili kwa Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi kutoka Taasisi na Halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Arusha.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taaluma (PSPTB) Amos Kazinza akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Uongozi wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi(PSPTB) kwa mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Missaile Musa
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma ( PSPTB) Shamim Mdee akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili kwa Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi kutoka Taasisi na Halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Arusha.
Mkuu wa kitengo cha Ununuzi (PSPTB) Absalom Nnko akiwasilisha mada kuhusu sheria mpya mafunzo ya siku mbili kwa Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi kutoka Taasisi na Halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Arusha.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Missaile Musa(katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa PSPTB wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji (PSPTB), Bw. Godfred, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, John Kayombo(wa kwanza kushoto waliokaa) pamoja na baadhi ya wakuu wa vitengo vya Ununuzi na Ugavi kutoka Taasisi na Halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Arusha
No comments:
Post a Comment