HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 25, 2024

KONGAMANO LA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA UBELGIJI KUVUTIA WAWEKEZAJI

 

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo akizungumza leo Novemba 25, jijini Dar es Salaam wakati wa kongamano la Uwekezaji.

KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini Tanzania (TPSF) wameandaa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Ubelgiji ambalo linalengo la kukuza uwekezaji Tanzania.

Sekta za kipaumbele katika jukwaa hili ni pamoja na Utalii, Madini, Viwanda, Kilimo, Ujenzi na Nishati.

Akizungumza leo Novemba 25, jijini Dar es Salaam wakati wa kongamano hilo,Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo amesema kuwa Mkutano huo utasaidia kubadilishana mawazo kwa lengo la kutambua fursa zilizopo nchini.

Amesema mkutano huo umewakusanya wawekezaji 40 kutoka nchi ya Ubelgiji na wafanyabiashara kutoka Tanzania zaidi ya kampuni 300.

"Wawekezaji kutoka Ubelgiji wanaweza kichukua nafasi kuwekeza hapa Tanzania lakini kutengeneza urafiki na Watanzania." Amesema Dkt. Jafo

"Imani yetu kubwa na kwa dhamira ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kuvutia Wawekezaji, jambo hillo lnafanikiwa na malengo ni kuufikia uchumi wa Viwanda." Ameeleza.

Amesema kuwa Tanzania inatafanya vizuri na mwisho wa siku tukuze pato la taifa lakini pia kutengeneza ajira kwa wananchi.

Dkt. Jafo amesema kuwa Ulali wa biashara umekwenda vizuri katika miaka ya hivi karibuni kwani Tanzania tunasafirisha bidhaa za Dola za Marekani milioni 186 nchi ya Ubelgiji wamesafirisha bidhaa zaidi ya dola za kimarekani milioni 115.

Kwa upande wa Balozi Tanzania nchini Ubelgi, Jestas Nyamanga amesema kuwa wamekuja nchini na ujumbe wa watu 40 ambao ni wafanyakazi, wafanyabiashara na wawekezaji kampuni 40 na vyombo mbalimbali vinavyosukuma Uwekezaji nchini Ubelgiji.

"Tuko hapa kuangalia fursa na kuona namna gani tunavyoweza kuwekeza Tanzania na mpaka sasa Uwekezaji wao unafikia dola za kimarekani 430 na uwekezaji huo upo katika sekta za kilimo, Nishati, Madini na Hoteli.

Tumekuja ili tuweze zaidi kwenye sekta nyingine hasa sekta ambazo zinaendelea kukua Tanzania. Amesema

Nyamanga amesema kuwa Ubelgi ni nchi mojawapo katika bara Ulaya ambapo Tanzania wanauza kuliko tunavyonunua kwao.

"Kwa sasa karibu kila mwaka dola kimarekani zaidi ya 185 na wao wanauza karibu nusu ya fedha hiyo." Amesema

Licha ya hayo Nyamanga amesema kuwa watatembelea maeneo mbalimbali ya uwekezaji nchini kwa lengo la kuona Tanzania katika maeneo ya wekeza nchini.

Akizungumzia Kongamano hilo, Kaimu Mkurugenzi, Uhamasishaji Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC), Daud Liganda amesema kuwa ni kongamano lililowaleta pamoja sekta binafsi na ujumbe wa Ubelgiji.

Amesema ujio wa Ujumbe huo ni neema kwa sababu wakifanya jitihada na juhudi za kuvutia uwekezaji kutoka nchi mbalimbali.

"Tunatarajia mara baada ya mkutano huu wawekezaji kutoka Ubelgiji utaongezeka kwa sababu uwekezaji wa nchi hiyo hauridhishi." Amesema

Ameeleza kuwa Katika miaka miaka yote kuanzia 1997 mpaka oktoba TIC imeandikisha miradi 48. Miradi hiyo kwa miaka 20 ni uwekezaji ambao hautoshi.

Kupitia kungamano hili utakwenda kuamsha Kampuni nyingi zaidi ya uwekezaji katika sekta mbalimbali kuja kuwekeza hapa nchini.

"Uwekezaji huo wa kampuni 48 umeweza kutengeneza ajira 2000 na unadhamani ya dola za kimarekani 2000 ikiwa hazitoshi ukilinganisha na nchi nyingi ambazo zimeona kuwa Tanzania ni mahali sahihi pa uwekezaji." Amesema



Baadhi ya Wadau wa Uwekezaji wakiwa katika Kongamano jijini Dar es Salaam leo Novemba 25, 2024.


Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Ubelgiji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad