HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 26, 2024

KEVOWAC si Chuo cha kufundisha masomo ya Afya-NACTVET

 

Meneja wa Udhibiti Ubora wa NACTVET Mhandisi Enock Kayaani akizungumza kuhusiana na Chuo cha KEVOWAC kilichofungwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda.
NACTVET wakiangalia mazingira ya Chuo hicho kusichokuwa na usajili

Afisa Mtendaji wa Nzasa Hilda Kalolela akizungumza kuhusiana na chuo hicho kuendelea kuwa wanafunzi wakati kikiwa kimefungwa.


*Ni Chuo ambacho hakina usajili wa NACTVET

Na Chalila Kubuda,Michuzi TV
KUFUATIA na kufungwa kwa Chuo cha Afya cha KEVOWAC na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda ,Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) imefika katika Chuo hucho na kubaini hakina hadhi ya kuwa Chuo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupata taarifa kupitia vyombo vya Habari Meneja wa Udhibiti Ubora wa NACTVET Mhandisi Enock Kayaani amesema kuwa Mkuu Wilaya kukifunga Chuo hicho jambo la msingi katika mstakabali wa elimu nchini.

Kayaani amesema kuwa katika mazingira ya Chuo hicho hayaridhishi licha ya kufungiwa lakini vijana wameendelea kukaa hapo wakati hakina uwezo wa kufundisha masomo ya afya.

Amesema anatilia shaka vijana waliopo katika chuo hicho kuwa hawana vigezo vile ambavyo vinahitajika katika kusoma kozi ya afya.

"Mazingira waliopo vijana hayastahili katika kupata elimu huku akihoji wazazi kwa nini wamewapeleka vijana wao katika chuo ambacho hakina vigezo vya kuitwa chuo"amesema Mhandisi Kayaani.

Hata hivyo amesema kuwa wazazi wakitaka kupeleka vijana wao waingie tovuti ya NACTVET na kuangalia orodha ya vyuo vilivyosajiliwa vitavyofanya vijana wapate elimu sitahiki.

Amesema Mkurugenzi wa Chuo alipowasiliana anasema anafatilia taratibu kuhusiana na chuo hicho licha ya kufungwa lakini bado wanafunzi wako katika hosteli.

Afisa Mtendaji Adela Kalolela amesema kuwa wazazi wanawajibu kufika vyuo wanavyosoma vijana katika kujiridhisha.

Amesema kuwa vijana wanasoma baadae wanapokuwa wamehitimu wakiomba kazi wanaambiwa chuo alichosoma hakitambuliwi huku mzazi kashalipa ada.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad