Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wamepongezwa kwa kuendelea kufanya Baraza la Wafanyakazi lenye tija linaloendelea kuwa chachu ya maamuzi makubwa ya kuboresha uboreshwaji wa huduma za Usafiri wa Anga nchini.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Salim Msangi wakati wa ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi la TCAA uliofanyika Novemba 14, 2024 jijini Dar es Salaam.
Bw. Msangi ameongeza kuwa, kufanyika kwa vikao hivyo vya Baraza ni kuimarisha demokrasia mahala pa kazi,na kuwataka wajumbe wa Baraza hilo kurudisha mrejesho kwa watumishi wenzao na kuwahimiza kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuendelea kutenda kazi kwa ufanisi.
"Menejimenti inatambua mchango wa kila mtumishi kwa taasisi na ni vyema kila mmoja akatambua TCAA inajengwa kwa kuianzia na wewe, nawasihi sana tufanye kazi kwa kushirikiana na inapobidi msaidie mwingine ili kuhakikisha malengo ya taasisi na serikali kwa ujumla yanafikiwa na huduma inatolewa" amesema Bw. Msangi.
Pamoja na majadiliano wajumbe wa baraza walipata nafasi ya kusikiliza wasilisho kuhusu akili ya kihisia “Emotional Intelligence” kutoka kwa Dkt. John
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la TCAA wakati wa kufungua kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi akiongoza kikao cha Baraza la Wafanyakazi la TCAA wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Katibu wa Baraza Bw. Mweya Dedacus na kulia ni Katibu Msaidizi wa Baraza Neema Matagi.
Wajumbe wa Baraza wakiendelea kufuatilia mada katika kikao hicho
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la TCAA wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment