Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi anatarajiwa kuongoza waombolezaji katika shughuli ya kutoa heshima za mwisho na mazishi ya Ndugu Christina Alex Kibiki, aliyekuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa, ambaye alipoteza uhai hivi karibuni baada ya kuvamiwa na kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana.
Katibu Mkuu Balozi Nchimbi ambaye amewasili tayari mkoani Iringa kwa ajili ya shughuli hiyo, itakayofanyika leo Ijumaa, tarehe 15 Novemba 2024, katika Kijiji cha Banavanu, njia panda Tosamaganga, ataambatana na Mjumbe wa Kamati Kuu, Ndugu Haji Gavu, ambaye ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM – Oganaizesheni, pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali Mkoa wa Iringa.
Ndugu Kibiki alipoteza uhai usiku wa tarehe 12 Novemba 2024, katika tukio hilo la kikatili, baada ya kuvamiwa na kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake usiku huo, ambapo hadi sasa wahusika wa unyama huo bado hawajajulikana, huku vyombo vya dola, kupitia jeshi la polisi, vikiendelea kuwasaka kwa ajili ya hatua za kisheria.
Kabla ya kuelekea kijijini Banavanu kwa ajili ya mazishi, Balozi Nchimbi atajumuika pamoja na waombolezaji wengine katika ibada ya mazishi ya marehemu Ndugu Kibiki, itakayofanyika katika Kanisa la Romani, Tosamaganga.
Friday, November 15, 2024
Home
Unlabelled
BALOZI NCHIMBI KUONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA KIBIKI LEO
BALOZI NCHIMBI KUONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA KIBIKI LEO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment