Kampuni ya Airplanes Africa Limited (AAL) yenye makao yake Morogoro, imetangaza kuwa ndege tatu za kwanza zilizotengenezwa Tanzania, zinazojulikana kama Skyleader 600, zimeanza rasmi safari zake ndani na nje ya nchi.
Mkurugenzi wa
AAL, Bw David Grolig amesema kuwa ndege moja kati ya hizo tatu imetua
kwa mara ya kwanza kwenye uwanja Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
ikiwa sehemu ya uzinduzi wa kuanza kufanya kazi.
Bw Grolig
alithibitisha kuwa kampuni yao imepata kibali kwa mamlaka husika na
msuala ya usafiri wa anga na hiyo imefanyika baada ya kuthibitisha ubora
wake.
Alisisitiza kuwa ndege ya Skyleader 600 ni ya kisasa, ina
ubora wa hali ya juu na inakidhi viwango vyote vya kimataifa na
kuruhusiwa kuanza kufanya kazi.
"Tumetengeneza ndege tatu aina ya
Skyleader 600 hapa Tanzania, na sasa ziko tayari kuuzwa. Ndege hizi
zinatoa suluhisho bora la usafiri kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla, na
tunakaribisha wateja wanaopenda kumiliki," alisema Bw Grolig.
Alifafanua
kuwa uamuzi wa kuanzisha kiwanda cha utengenezaji wa ndege nyepesi
Tanzania ulitokana na mazingira mazuri ya uwekezaji nchini na utayari wa
wananchi kukubali teknolojia na kujifunza ujuzi mpya.Alisema kuwa ndege
hiyo inabeba abiria wawili, pamoja na rubani na inafaa sana kwa
wasafiri wa kibiashara wanaofanya safari za umbali mrefu.
"Tulifanya
utafiti wa kina kuhusu mahitaji ya wasafiri wa kibiashara ambao mara
kwa mara husafiri kwa umbali mrefu. Kutokana na utafiti huo,
tulitengeneza ndege ambayo inawawezesha wafanyabiashara kusafiri kwa
ufanisi na kuhudhuria mikutano mbalimbali nje ya maeneo yao kabla ya
kurejea mjini,” alisema.
AAL ni kampuni ya kwanza Tanzania
kutengeneza ndege za aina hii kwa matumizi ya kibiashara na binafsi na
pia ikichangia soko la ajira nchini.
Alifafanua kwa kusema kuwa gharama za kununua ndege hizo ni nafuu kama kumiliki gari.
"Mafanikio ya mradi huu yanatokana na jitihada za pamoja na za kujituma za timu yetu ya Kitanzania na Czech," alisema.
Ndege
hiyo ilioneshwa hivi karibuni katika Maonyesho ya Watengenezaji wa
Bidhaa ya Tanzania (TIMEXPO 2024) yanayoendelea katika Maonyesho ya
Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF).
TIMEXPO 2024,
yaliyoandaliwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kwa kushirikiana
na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), yamevutia zaidi
ya kampuni 300 za ndani na kimataifa.
Ndege ya kwanza iliyotengenezwa nchini Tanzania, Skyleader 600, ikitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1) kwa mara ya kwanza katika historia. Ndege hiyo imetengenezwa na kampuni ya Airplanes Africa Limited (AAL) yenye makao yake Morogoro na inafaa kwa usafiri ndani ya Tanzania na kimataifa.
Mkurugenzi wa Airplanes Africa Limited (AAL) AAL, Bw David Grolig (kushoto) akipozi na mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo mara baada ya ndege hiyo kutua kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1) kwa mara ya kwanza katika historia.
Ndege ya kwanza iliyotengenezwa nchini Tanzania, Skyleader 600, ikiwa imesimama kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1) kwa mara ya kwanza katika historia. Ndege hiyo imetengenezwa na kampuni ya Airplanes Africa Limited (AAL) yenye makao yake Morogoro na inafaa kwa usafiri ndani ya Tanzania na kimataifa.
Ndege ya kwanza iliyotengenezwa nchini Tanzania, Skyleader 600, ikitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1) kwa mara ya kwanza katika historia. Ndege hiyo imetengenezwa na kampuni ya Airplanes Africa Limited (AAL) yenye makao yake Morogoro na inafaa kwa usafiri ndani ya Tanzania na kimataifa.
Wafanyakazi wa kampuni ya Airplanes Africa Limited (AAL) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Ndege hiyo aina ya Skyleader 600,kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1) kwa mara ya kwanza katika historia.
No comments:
Post a Comment