HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 10, 2024

Mgalu afunguka mafanikio ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan

-Diwani Kata ya Dunda aweka silaha za ushindi uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Na Chalia Kibuda ,Michuzi Blog

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani CPA Subira Mgalu amesema serikali ya awamu ya Sita chini Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imetekeleza Ilani ya Chama kwa asilimia 100 hivyo anahitaji kuungwa mkono katika chaguzi mbalimbali ikiwemo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Mgalu ameyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Kata ya Dunda ulioandaliwa na Diwani wa Kata hiyo Amiri Mpwimbwi kwa ajili ya kuwaaga vinyeviti wa vitongoji katika kutekekeza kwa vitendo maendeleo ya kata hiyo.

Mgalu amesema kuwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amedhihirisha utendaji wa ilani na kufanya kuwa na fomu moja tu ya mgombea Urais 2025.

Aidha amesema kuwa maendeleo yaliyofanyika kwa viongozi kuonyesha katika ushindani wa uchaguzi wa serikali mitaa kwa kuhakikisha viongozi wa CCM wanaendelea kushikiria rekodi ushindi ambayo ndio furaha yake Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Katika Mkutano huo Mbunge huyo alitoa mipira 20 pamoja na Jezi Pea 10 kwa ajili ya kuandaa vipaji kwa vijana wa kata hiyo .

Hata hivyo alichangia tofali 2000 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni katika shule ya sekondari katika kata ya Dunda pamoja aliweza kuahidi kuwa na ofisi ya Jukwaa la Uwezeshaji wa Kiuchumi.

Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Dunda Amiri Mpwimbwi amesema kuwa wametekeleza ilani ya chama ya kufikisha maendeleo.

Amesema miradi yote iliyofanyika katika kata ya Dunda zaidi bilioni 8 katika maeneo ya Barabara ,Maji ,Umeme pamoja na elimu.
 

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani Subira Mgalu akizungumza  katika Mkutano wa Hadhara ulioandaliwa na Diwani  wa Kata ya Dunda Amiri Mpwimbwi uliofanyika Viwanja vya Top top mjini Bagamoyo
 

Diwani wa Kata ya Dunda Amiri Mpwimbwi akizungumza katika mkutano akiwa na viongozi wa vitongoji wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo katika kata hiyo.
 

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani Subira Mgalu akikabidhi Jezi Pea 10 na Mipira 20 kwa viongozi wa Kata ya Dunda akiwemo Diwani wa Kata hiyo Amiri Mpwimbwi.
 

 Diwani wa Kata ya Magomeni,Wilaya Bagamoyo Mwanaharusi Jarufu akitoa salamu katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Diwani wa Kata ya Dunda Amiri Mpwimbwi.
 

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani Subira Mgalu akikaribishwa kuhutubia hadhara ya wananchi wa kata ya Dunda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad