Kawaida ametoa ufafanuzi na elimu hiyo wakati wa ziara yake wilayani Muleba alipokutana na kuzungumza na wananchi katika maeneo mbalimbali leo Oktoba 18, Mwaka huu ukiwa ni mwendelezo wa ziara yake mkoani Kagera yenye lengo la kuhamasisha uandikishaji wa wapiga Kura.
Akiongea katika kata za Runazi, Rulanda na Muleba Mjini, @comrade_kawaida amewataka wananchi kutofautisha uandikishaji huu wa makaazi na uandikishaji uliopita sambamba na kuwataka viongozi katika mikoa ambayo uandikishaji upo chini kutumia siku zilizobaki kutoa elimu kwa wananchi.
Hata hivyo Kawaida ameenedelea kuwahimiza wananchi ambao hawajajiandikisha kuendelea kutumia siku zilizobaki kujiandikisha ili kuweza kupata sifa za kupiga kura na kuwachagua viongozi bora watakao waongoza katika serikali za vijiji, Vitongoji na mitaa pamoja na wajumbe wao.
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba ni moja kati ya Halmashauri 8 za mkoa wa Kagera na ni wilaya yenye kata 43 ambapo ina vituo 802 na inakadiriwa kuandikisha wapiga kura laki tatu ambapo uandikishaji hadi sasa ni asilimia 46.4.









No comments:
Post a Comment