Pindi utakapojiandikisha utakuwa na uhakika wa kuchagua Kiongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27,2024 bado siku 1 imebaki wananchi kujiandikisha katika vituo mbalilmbali nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Martine Shigela amesema hayo wakati akikagua na kutembelea Vituo vya kujiandikisha Halmashauri ya wilaya ya Geita ambapo ametembelea vituo katika Kata za Nzera na Bugulula.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Karia Magaro amesema wanatarajia kuandikisha wananchi zaidi ya 500,124 ambapo hadi sasa zoezi la uandikishaji linaendelea na wanatarajia kufikia zaidi ya asilimia 50.
No comments:
Post a Comment