MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogogolo, leo anaendelea na ziara yake katika Jimbo la Segerea yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wanchi pia anapata fursa ya kuzungumza na viongozi wa mitaa kuanzia mashina mpaka wenyeviti hili kuwakumbusha juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea.
Mara baada ya mkutano wa ndani Mkuu wa Wilaya atasilikiliza kero za wananchi wa kata za Kipawa na Minazi Mirefu na kuwahutubia.
Katika ziara hii DC Mpogolo, ameambatana na wataalamu na wanasheria kutoka ofisi yake na Ikulu waliotumwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Wananchi wote wenye kero, maoni na ushauri wanaarifiwa kufika na kuonana na DC katika mkutano wa hadhara utakaofanyika saa 9: alasili.
No comments:
Post a Comment