HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 11, 2024

WMA kutoa gawio la sh. Bilioni 7.7 mwaka wa Fedha 2025/2026

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) Alban Kihulla akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Habari katika Mkutano mwendelezo ya Mikutano inayoratibiwa na Msajili wa Hazina ,Jijini Dar es Salaam.

Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabato Kosuri akizungumza kuhusiana mikutano kati Mashirika ya Umma yaliyo chini ya Msajili wa Hazina na Wahariri wa Vyombo vya Habari
Wahariri na Waandishi wakipitishwa kuangalia uhalisia wa vipimo katika Mkutano ulioandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina Jijini Dar es Salaam.

*Yaweka mikakati ya kwenda kwenye vipimo vya vifurushi vya simu pamoja na michezo ya kubahatisha


Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
AFISA  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) Alban Kihulla amesema kuwa Wakala huo unatarajia kutoa Gawio la Serikali Sh.Bilioni 7.7 katika mwaka wa Fedha 20025/2026.

Kihulla ameyasema hayo wakati akizungumza na wa Wahariri na Waandishi katika Mkutano ulioandaliwa na Msajili wa Hazina na kufanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema katika miaka mitano wameendelea kutoa gawio katika kuhakikisha maendeleo yakapatikana kwa wananchi ambapo mwaka wa fedha 2018/2019 gawio la sh.Bilioni 4.2.,2019/2020 gawio la sh.bilioni5.3.,2020/2021 gawio la sh.bilioni6.2.,2021/2022 gawio la sh bilioni 4.2.,2022/2023 gawio la sh bilioni 4.3

Amesema hadi kufikia hapo WMA imepita hatua tofauti tofauti Kwa kuanzia Ukoloni ikiwa katika Idara ya Wizara ya Mambo ya Ndani ambapo sasa ipo Wizara ya Viwanda na Biashara.

Amesema majukumu ya WMA ni kumlinda mlaji kupitia uhakiki na udhibiti wa vipimo vinavyotumika katika biashara na huduma nyingine pamoja na kuhakikisha kuwa vipimo hivyo viko sahihi na vinatumika kwa usahihi kulingana na sheria ya vipimo.

Amesema kuwa wameendelea kutoa elimu kuhusiana na vipimo na kuwa na Ofisi katika mikoa yote ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya vipimo na pale wanapowazika kutoa taarifa.

Kihulla amesema kuwa wamejenga Ofisi Mkoa wa Pwani wa Kupima Mita za Maji ,Mita za Umeme pamoja na kupima matanki ya mafuta yanayoenda mikoani na nchi jirani Mafuta katika kupata uhalisia wa ujazo.

Aidha amesema wameweka mikakati mbalimbali ambapo mikakati hiyo wamejenga jengo la Makao Makuu jijini Dodoma pamoja na kuendelea kuelimisha wananchi kuhusiana na vipimo ambao ndio walaji wa mwisho.

Amesema kuwa mpango mwingine ni kwenda katika michezo ya kubahatisha vipimo vinavyotumika pamoja na vifurushi vinavyotolewa na Mitandao ya Simu za Mkononi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad