WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso, ametoa pongezi kwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) , Simiyu, Emmanuel Silanga kwa kujenga kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji kinachojulikana kama Moli Oil Mills.
Kiwanda hicho kipo mtaa wa Majahida wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, jambo ambalo Waziri huyo alisema linasaidia kuleta maendeleo katika jamii.
Waziri Awesome aliyazungumza hayo wakati wa ziara yake ya kwenda kukagua mradi huo, alifurahishwa na utendaji kazi wa Gungu kujenga kiwanda hicho mkoani Simiyu, ikiwa ni tofauti na wamiliki wengi wa viwanda hufikiria kuviweka jijini Dar es Salaam.
“Nampongeza Kaka yangu kwa kutekeleza maono ya Rais Samia kwa vitendo, uanzishwaji wa kiwanda hiki utasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana kwani wana Simiyu wengi wataajiriwa hapa na pia ujenzi wa mradi wa maji ya ziwa Victoria utatumia mabomba hayo, hivyo ametumia fursa kwa wakati sahihi.
Aliongeza "Angeweza kujenga kiwanda hicho jijini Dar es Salaam ama kwingine, lakini kaamua kuwa mzalendo kwa kukumbuka nyumbani kwanza, hivyo ajira zitamwagika kwa wingi kwani ni kiwanda cha kisasa, nawaomba na wawekezaji wengine kujenga viwanda zaidi mkoani hapa, jambo ambalo litapunguza vijana kukosa ajira".
Kwa upande Gungu alimshukuru, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu kwa kuweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara na wawekezaji, jambo linalowapa moyo wa kuendelea kupambana kutekeleza ilani ya chama cha CCM.
"Rais wetu ameweka wepesi wa wawekezaji kufanya kazi kwa moyo na kujituma kwa bidii," alisema.
Wakati wa ziara hiyo Waziri Aweso aliambatana na Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Bariadi, Andrea Kundo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kenani Kihongosi na Mbunge wa Viti Maalum Lucy Sabu..
No comments:
Post a Comment