Ujumbe huo umekuja kumpatia mrejesho wa ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Benki ya Dunia hasa katika uhifadhi wa maliasili na utekelezaji wa mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW)ikizingatiwa kwamba Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) ameteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuiongoza Wizara hiyo.
Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Chana ameishukuru Benki ya Dunia kwa namna ambavyo imeendelea kuiwezesha Tanzania kwenye juhudi zake za uhifadhi na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshugulikia maliasili, Kamishna Benedict Wakulyamba na Mratibu wa Mradi wa REGROW, Aenea Saanya.






No comments:
Post a Comment