Mhe. Rais Dkt. Samia ameendelea kusisitiza kauli yake ya kuwashukuru wakulima wa Ruvuma na maeneo yote nchi nzima kwa jinsi juhudi zao zimeendelea kuifaharisha nchi kwa usalama wa chakula huku ziada ikitunzwa, nyingine kuuzwa nje ya nchi na kuwa mojawapo ya vyanzo vya pato la taifa na mapato ya fedha za kigeni.
Mbali na kuwashukuru kwa juhudi na ushirikiano wa wakulima, Mhe. Rais Dkt. Samia pia amesisitiza kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi anayoiongoza, itaendelea kutimiza wajibu wake kuwahudumia wakulima hao, hasa kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo, zikiwemo mbolea, huduma za ugani, mbegu bora na masoko ya mazao yao, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 - 2025.






No comments:
Post a Comment