HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, September 8, 2024

POLISI YAONGEZA NGUVU UCHUNGUZI TUKIO LA MAUAJI

 


Jana Septemba 7,2024 Jeshi la Polisi lilitoa taarifa juu ya Ally Mohamed Kibao kushushwa kutoka kwenye basi la Tashrif na kuchukuliwa na watu ambao hawakuweza kutambuliwa na kwamba uchunguzi ulianza baada ya kupokelewa taarifa hiyo.

Baada ya kutolewa taarifa za kuonekana mwili wa mtu mwanaume ambaye hakuweza kutambuliwa kwa wakati huo ni mwili wa nani huko Ununio Jijini Dar es Salaam, utambulizi umefanyika kwa mujibu wa taratibu na kubainika ni mwili wa Ally Mohamed Kibao.

Aidha, uchunguzi wa mwili wa marehemu (postmortem) umefanywa leo tarehe 08/09/2024 na Madaktari bingwa kwa kushirikisha familia.

Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hili la kusikitisha na timu ya uchunguzi wa matukio makubwa toka Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai toka Makao Makuu imetumwa kuongeza nguvu kwenye timu ya awali ili kuhakikisha waliofanya mauaji haya wanakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za kweli na za uhakiki aziwasilishe kwa mujibu wa taratibu ili kusaidia kufanikisha kukamilika mapema kwa uchunguzi wa tukio hili la kusikitisha.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad