HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 16, 2024

MWANANCHI NI MLINZI NAMBA MOJA WA AMANI

 

Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA ameiomba jamii ya Watanzania kuwa walinzi namba moja kulinda na kutoa taarifa za viashiria vya uvunjifu wa amani kwa kushirikiana na vyombo vya dola kwakuwa jukumu la kulinda amani ni la wote.

MAJALIWA amesema hayo leo 16 Septemba katika Baraza la Maulid Kitaifa Ukumbi wa Shule ya Sekondari Wasichana ya NYANKUMBU iliyopo Halmashauri ya Mji wa GEITA na amewataka Watanzania tujiulize kwanini matukio ya uhalifu yanatokea kukaribia vipindi vya uchaguzi.



'Kila Mtazania anawajibu wa kulinda na kusimamia amani ya nchi na kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vya uvunjifu wa amani kwa kushirikiana na vyombo vya dola kwakuwa jukumu la kulinda amani ni la wote na waache kunyooshea kidole Jeshi la Polisi pekee.' Amesema MAJALIWA

Wakati akitoa salamu za Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA ALHAJ NUHU MRUMA amesema Baraza hilo imelaani na kukemea vitendo vya uvunjifu wa amani na kuiomba serikali kufuatilia kwa kina vitendo hivyo.

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dkt. ABUBAKARY ZUBERI BIN ALLY amesema kila mwislamu wakati wa kuadhimisha Maulid ya Mtume MUHAMMAD [S.A.W] watende mema na wayaishi maisha ya Mtume MUHAMMAD na wawe wazalendo katika nchi yao kwakuwa hakuna sehemu mbadala pa kwenda hivyo wana wajibu wa kuipenda na kuilinda nchi yao.



Wakati huo huo baadhi ya taasisi zilizoshiriki katika Baraza la Maulid Taifa Mkoani GEITA ni taasisi ya Kifedha Benki ya CRDB salamu za Benki hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB ABDULMAJID NSEKELA,Meneja wa Biashara Islamic Banking THABIT GALIA amesema benki hiyo inajivunia kuwa sehemu ya Baraza la Maulid lakini kuwa moja ya sehemu ya jamii inayojali imani na mahitaji ya wateja wote kwasababu hiyo wana bidhaa maalum ya ISLAMIC BANKING kupitia nembo mahususi ya AL - BARAKAH imetengenezwa kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya kifedha kwa wateja wa kiislamu kwa kufuata misingi ya Sharia kutokana na wateja hao kuhitaji kupata huduma za kifedha zenye uwazi,haki na ambazo zinawiana na imani yao.



'Benki ya CRDB itaendelea kuwa bega kwa bega na jamii yetu ya Kiislamu na tutahakikisha kuwa tunatoa huduma za kifedha zinazojali na kuheshimu misingi ya dini na hadi sasa wananchi zaidi ya 200,000 wameshajiunga na huduma hiyo ya AL - BARAKAH BANKING'. Amesema GALIA


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad