Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) Bw. Plasduce Mbossa, Septemba 9, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Shirika la Meli la COSCO la nchini China Bw. YangFan Chen kuhusu kuimarisha mashirikiano ya kibiashara baina ya TPA na COSCO.
Katika mazungumzo hayo Viongozi hao wamejadili namna bora ya kushirikiana ili kuongeza ufanisi katika kutoa huduma za Shehena zinazoingia na kutoka Nchini.
Bw. Chen ameambatana na watendaji waandamizi wa kampuni hiyo na kutembelea maeneo mbalimbali ya kutolea huduma Bandarini, ameahidi kuendeleza ushirikiano na TPA ili Wateja wao kupata huduma kwa haraka.
No comments:
Post a Comment