Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu mbili ambazo ni Femtech na Kuza femtech ambazo zitawasaidia wanawake. uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leeo Septemba 10, 2024.
KATIKA kuwasaidia Wasichana na Wanawake kumudu maisha na kuisaidia jamii Tume ya Sayansi na Teknolojia ( Costech), imezindua Program mbili kwa ajili ya kuwajengea uwezo kidijitali.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 10, 2025 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Dkt. Amos Nungu amesema kuwa Program hizo ni kwa ajili ya wasichana ambao hawakumaliza masomo yao na Wanawake wenye mawazo au biashara zinazohusiana na Teknolojia.
Lengo ni kuwapa ujuzi na taaluma ya kiteknolojia ili waweze kuja na biashara ambazo zinaweza zikasaidia waweze kumudu maisha yao, na wasaidie jamii.
Dkt. Nungu amesema Program ya kwanza inajulikana kama 'Future Femtech' inayowasaidia wanawake wenye kampuni changa au mawazo machanga ya kiteknolojia.
Amesema Program ya pili ijulikanayo kama 'Kuzatech' inaangalia mabinti ambao walikuwa shule lakini kwa namna moja au nyingine wakashindwa kuendelea na masomo hivyo wamewapa fursa ya kupata mafunzo kidijitali.
"Sasa hizi Program mbili tunazifanya kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo,"amesema.
Nungu amesema Kuzatech wataunganika na Future Femtech ambao baadhi yao ni wahitimu wa vyuo vikuu wenye mawazo ya biashara ambapo wadogo wanapata fursa ya kuungana na hawa wakubwa ili waweze kupata mafunzo yatakayowasaidia kuwa nankitu cha kufanya.
Kwa upande wake Meneja Usimamizi na Uhaulishaji Teknolojia Costech, Dkt. Erasto Mlyuka amesema Program hiyo ya Future Femtech inawalenga wasichana ambao wamekuwa ni waanzilishi wa kampuni changa.
Amesema hupewa msaada wa kitaalam kwa maana ya mafunzo elekezi ya kujengewa uwezo pia kupewa fedha za kuwawezesha kufanya biashara zao.
Amesema program hizo zitatengeneza ajira kwa wanawake ili na wenyewe wapate nafasi ya kuchangia kwenye pato la nchi kwa kuwa na kipato halali.
Mbunifu kutoka Arusha, ambaye ni mnufaika wa Future Femtech, Pamela Chogo amesema mafunzo aliyoyapata ni chachu kubwa kwenye ubunifu wa biashara.
Amesema Program hizo ni muhimu kwa sababu zinasaidia kupata elimu ya ujasiriamali.
Meneja Usimamizi na Uhaulishaji Teknolojia Costech, Dkt. Erasto Mlyuka akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu kwaajili ya wasichana na wanawake jijini Dar es Salaam leo Septemba 10, 2024.
Picha ya Pamoja
No comments:
Post a Comment