HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 23, 2024

WATENDAJI WA KATA, VIJIJI NA MITAA WAAGIZWA KUENDELEZA UHAKIKI ANWANI ZA MAKAZI


Na Mwandishi Wetu, WHMTH, Arusha

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Mwl. Husein Bakari amewaagiza Watendaji wa Kata na Mitaa wa jiji hilo kutimiza wajibu wao wa kuendelea kuhakiki taarifa za Anwani za Makazi na siyo kusubiri oparesheni kama inayoendelea sasa jijini humo.

Mwl. Husein ambaye pia ni Afisa Elimu amesema hayo leo tarehe 23 Agosti baada ya kupokea ripoti ya maendeleo ya zoezi la Uhakiki wa taarifa za Anwani za Makazi wakati alipokutana na timu ya Waratibu wa Anwani za Makazi Taifa, Mkoa na Wilaya katika ofisi za jiji.

Akitoa taarifa fupi, Msimamizi wa zoezi la Uhakiki Jiji la Arusha Bw. Medson Naftari amesema, tangu kuanza kwa zoezi hilo tarehe 16 Agosti hadi leo, wamefanikiwa kusasisha taarifa za anwani 32,605 sawa na asilimia 21.35 ya anwani zilizopo ndani ya jiji ambazo ni 152,750.

Amesema anwani ambazo bado hazijahakikiwa ni 120,145 wakati anwani mpya zilizosajiliwa ni 2,448 sawa na ongezeko la asilimia 1.6 


Baada ya kupokea ripoti hiyo Kaimu Mkurugenzi huyo wa Jiji la Arusha amesema kuwepo kwa idadi ya Anwani mpya Nnn kunadhihirisha wazi kuwa baada ya uhakiki uliofanyika kwa jiji hilo mwaka 2023 kulikuwa na ulegevu/udumavu kwa Watendaji wa Kata na Mitaa katika uendelezaji wa uhakiki kwa kila anwani mpya.



Mwl. Husein amemwagiza pia Kaimu Mratibu wa Anwani za Makazi kwa jiji la Arusha, kuhakikisha anafuatilia mzabuni aliyepewa tenda ya kutengeneza nguzo za majina ya barabara ili barabara ambazo hazina nguzo ziwekewe sanjari na maeneo ambako miundombinu hiyo imeharibiwa.

Kwa upande wake Mratibu wa Anwani za Makazi Taifa, Mhandisi Jampyon Mbugi amemuomba Kaimu Mkurugenzi huyo pamoja na viongozi wengine kutumia kila fursa wanayoipata kutoa elimu ya umuhimu wa Mfumo wa Anwani za makazi na matumizi yake kwa manufaa ya taifa zima.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad