Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Hassan Mwinyikondo.
Na Khadija Kalili Michuzi Tv
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani Hassan Mwinyikondo ametoa rai kwa wataalamu na taasisi mbalimbali kushuka chini kwa wananachi kwenda kuwasikiliza na kukamilsha miradi mbalimbali.
"Ni jukumu lenu kushuka chini kwa wananchi kwenda kiwasikiliza na kuwatatulia kero zao, nawasihi sana Waheshimiwa Madiwani wawaandalie mikutano nanyi mje mzungumze na wananchi kama jinsi wanavyofanya TAKUKURU wao hukutana na wananchi katika mikutano na wananchi na kupokea kero zao na kuzitafutua utatuzi." Amesema Mwinyikondo
Akizungumza katika kikao cha Madiwani Chalinze robo ya nne Mwenyekiti Hassan Mwinyikondo amesema kuwa "Chalinze tumejipanga kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo kujenga Kituo Cha mafuta 'Petrol Station' kwa ajili ya kuongeza vyanzo vya mapato ya ndani ya Halmashauri.
Mwinyikondo amesema kuwa pia wamepanga kuboresha huduma kwa wasafiri katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Chalinze kwa kuongeza kujenga vyoo kituo cha mabasi cha ikiwa ni katika kuboresha utoaji huduma kwa abiria.
Taarifa hiyo imetolewa Agosti 6, katika kikao cha Baraza la Madiwani Cha Kota ya nne ambacho kimemalizika kwa asilimia 100, amesema Mwinyikondo
Aidha Mwinyikondo amewasisitiza wataalamu wote kushirikiana na Madiwani katika kutekeleza miradi iliyopo sanjari na kuikamilisha kabla ya uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani.
"Madiwani na Wataalamu tunakwenda kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa hivyo ni wajibu wenu kushuka chini kwa wananchi mkatatue kero zao." amesema Mwinyikondo.
Kuhusu ukarabati wa Kituo Cha Afya Lugoba ambacho kilianza 1972, kutokana na uchavu wake tunatarajia kukifanyia ukarabati tumeomba gari na tunatarajia utaanza Septemba mwaka huu,"Tumeomba gari hivyo tunatarajia kukifanyia ukarabati na kukiboresha kiwe cha kisasa zaidi" amesema.
Aidha ameziomba Taasisi mbalimbali kutoa taarifa zao mapema kwa Baraza la Madiwani Chalinze ili waweze kupitia kwa wakati.
Akijibu hoja kuhusu kupelekwa umeme katika Shule ya Ridhiwani Kikwete , Meneja TANESCO Chalinze Salima Muharam amesema kuwa watapigania ndani ya mwaka huu ili shule hiyo ipate umeme.
"Tayari mkandarasi ameshapewa mikataba na tayari imepelekwa kwa Mwanasheria Mkuu baada ya hapo kazi itaanza haraka.
Baadhi ya Madiwani wakiwa katika Baraza hilo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze Ramadhan Possi
No comments:
Post a Comment