HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 23, 2024

WAFANYABIASHARA WA KATORO WAKOSHWA NA MABADILIKO YA SHERIA ZA KODI



Na Mwandishi wetu,

Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara kutoka Mamlaka ya Mji Mdogo Katoro Peter Sanga amesema wameridhishwa na mabadiliko yaliyofanyika kwenye Sheria za kodi Nchini na kumaliza mfumo wa Kodi kandamizi. 

Sanga amesema hayo wakati akizungumza katika halfa maalum ya utoaji wa elimu kwa mlipa kodi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) katika eneo la Mamlaka ya Mji wa Katoro ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Geita.

Amesema mabadiliko hayo yameondoa mgongano kati ya wafanyabiashara na TRA na kutoa mwelekeo mzuri unaowahamasisha wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiari kwa maendeleo ya taifa.  




Kwa upande wake Meneja wa Elimu kwa mlipa kodi kutoka TRA, Paul Walalalaze amesema serikali inaendelea kufanya mabadiliko katika Sheria ili kumfanya kila mtanzania kuinuka kiuchumi. 

Walalaze amesema TRA imejidhatiti kuimarisha ukaribu na wafanyabiashara ili kuwaogezea uelewa juu ya mbinu sahihi za kulipa kodi kwa wakati sambamba na kuinua biashara zao.




Mmoja wa wafanyabiashara wa Katoro akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro iliyopo Halmashauri ya wilaya ya Geita, Simon Kasatu amesema licha ya kuridhishwa na mabadiliko yaliyofanywa na serikali wameiomba TRA kuendelea kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa ajili ya kuwainua wafanyabiashara wadogo kiuchumi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad