Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akifafanua jambo
Na Khadija Kalili Michuzi Tv
WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mjini TARURA wamesaini mkataba wa ujenzi wa barabara katika viwango tofauti na Kampuni 25 za Wakandarasi Mkoani Pwani.
Hafla hiyo ya utiaji sani imefanyika leo Agosti 19 kwa kipindi cha 2024-2025 katika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Mkoa Pwani.
Meneja wa TARURA Mkoa wa Pwani Leopold Runji amesema kuwa fedha hizo zinatoka katika mifuko mbalimbali kama mfuko wa Barabara ambao utafanya matengenezo ya kawaida Km.810, matengenezo sehemu korofi Km338.56 matengenezo ya vipindi maalumu Km.77.34, ujenzi wa Makaravati mistari 80, ujenzi wa box culvert 3.
Mhandisi Runji amesema kuwa fedha za mfuko wa jimbo watatengeneza na kufanya ukarabati na ujenzi wa barabara mbalimbali kama ujenzi wa barabara za kiwango cha lami Km.1.35 barabara kiwango chachangarawe Km.52.15 ujenzi wa makaravati.
"Lengo kuu la TARURA Mkoa wa Pwani ni kuhakikisha kuwa mikataba yote itakayosainiwa na Wakandarasi wote kwa pamoja wanakwenda kuanza utekelezaji wa kazi hizi haraka iwezekanavyo
kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu zilizowekwa" amesema Mhandisi Runji.
Amesema kuwa kwa Mkoa wa Pwani bajeti ya fedha imeidhinishwa kutoka katika vyanzo mbalimbali iliwemo mfuko wa barabara jimbo ,tozo na mfuko wamaendeleo (Development RF) ambapo zote kwa jumla ni 31,475,786,735.93.
Runji amesema kuwa ofisi ya TARURA Mkoa wa Pwani imepokea maelekezo kutoka TARURA Makao Makuu kuhusu utekelezaji wa mpango wa manunuzi wa kazi za matengenezo ukarabati na ujenzi wa barabara 2024-25.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amewataka Wakandarasi hao kutekeleza kazi zao ikiwa ni pamoja na kukamilisha miradi kwa wakati na kwatika kipindi cha 2025 Dkt.Rais Samia Suluhu Hassan arakapopita asipokee malalamiko kutoka kwa wananchi nabadala yake apokee shukrani kwa kuufungua Mkoa wa kumaliza ujenzi wa barabara zote ambazo bado hazijalamilika.nawasihi mkaufungue Mkoa kabla ya lile jambo letu.
'Ninyi TARURA mnakauli mbou yenu isemayo Tumeifungua Mikoa hivyo nendeni mkaotekeleze ipasavyo kwani huwezi kuwa na maendeleo ya kiuchumi kama nchi hajafunguka na hii ni jitihada ya maendeleo na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi" amesema RC Kunenge.
Kunenge amesema kuwa "Nawapongeza kwa kujitokeza kufanya kazi hivyo fanyeni kazi kwa mujibu wa mikataba yenu sababu mmeomba wenyewe hii kazi"amesema Kunenge.
Aidha Kunenge amesema kuwa endapo Wakandarasi hao watapata changamoto katika utekelezaji wasisite kutoa taarifa katika ngazi za Wakuu wa Wilaya na vizuri na wao wakapata nakala ili waweze kufuatilia na kuulizia kwani hii mikataba siyo siri ndiyo maana inasainiwa eneo la wazi.
"Katekelezeni miradi na pindi inapotekelezwa wananchi wafahamu ili wapunguze malalamiko" amesema Kunenge.
Runji , amesema kuwa katika utekelezaji wake mfuko wa barabara (Road Fund) utatoa kiasi cha Sh.bilioni 7.5 na bilioni 14.5 zitatoka katika eneo la tozo ya mafuta na mfuko wa Jimbo utatoa Sh.bilioni 4.5 huku fedha za miradi ya maendeleo ya barabara Mil.milioni 300 na mfuko wa dharula utatoa Bil.1.9.
Meneja TARURA Runji amesema kwa awamu ya kwanza imesainiwa mikataba 25 yenye thamani zaidi ya Bil. 11.6 ikiwa ni sawa na asilimia 37 ya bajeti ya mwaka.2024-2025 huku katika awamu ya pili itasainiwa mikataba iliyosalia.
Akizungumza kwa niaba ya Kampuni Lusaka Qs.Amiri Mussa amesema kuwa watakwenda kuhakikisha wanamaliza kazi za ujeni wa barabara hizo ndani ya muda kama ilivyoelekezwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Tuesday, August 20, 2024
TARURA WASAINI MIKATABA YA BIL. 31 NA WAKANDARASI PWANI
Tags
# HABARI
# HABARI JAMII
HABARI JAMII
Labels:
HABARI,
HABARI JAMII
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment