HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 7, 2024

Rais Dkt. Samia Ateua wenyeviti wa bodi mbalimbali

  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, walioteuliwa ni kama ifuatavyo:- 


  1. Prof. Faustin Rweshabura Kamuzora ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Uwekezaji ya UTT – AMIS. Prof. Kamuzora ni Katibu Tawala wa Mkoa Mstaafu, anachukua nafasi ya Bw. Casmir Kyuki ambaye amemaliza muda wake; 


  1. Prof. Joseph Andrew Kuzilwa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP). Prof. Kuzilwa ni Profesa Mstaafu, Chuo Kikuu cha Mzumbe; na 


  1. Prof. Ahmed Mohamed Ame ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kwa kipindi cha pili. 

Uteuzi huu umeanza tarehe 04 Agosti, 2024.

Sharifa B. Nyanga
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad