HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 16, 2024

OSHA YAWANOA WAANDISHI WA HABARI WA DAR NA PWANI

 

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa kazi (OSHA), Khadija Mwenda akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu Usalama Mahala pa Kazi. Mafunzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 16, 2024 jijini Dar es Salaam.


Na Khadija Kalili, Michuzi Tv 
WAKALA wa Usalama na Afya Mahali pa kazi (OSHA), wamebainisha sababu za kuongezeka kwa magonjwa kazi ikiwemo misuli, mgongo , viuno na shingo kuwa yametokana na kutozingatiwa kwa usalama na afya maeneo mbalimbali ya kazi.

Mkurugenzi Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda amesema hayo leo Agosti 16, 2024 Jijini Dar es Salaam katika  wakati wa semina ya Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari (JOWUTA) ya siku moja  iliyowakutanisha zaidi ya washiriki 50 kutoka Dar es Salaam na Pwani.

“Mtindo wa ukaaji, viti vinavyotumika kwenye maofisi vinapaswa kuzingatia usalama na afya. 

"Ofisi husika zizingatie kanuni za Usalama na Afya mahali pa kazi  vinginevyo kuna athari kubwa  ya kiafya na kiuchumi katika maisha ya  baadaye kwa mfano kutumia fedha nyingi kwenye  kujitibu maradhi ambayo tunaweza kujikinga sasa" amesema Mkurugenzi  huyo.

Mwenda amesema hakuna mazingira ya kazi yasiyo na vihatarishi hivyo ni lazima Wakala hao kufanya ukaguzi wa mara kwa mara dhidi ya afya na usalama ili kuwalinda wafanyakazi dhidi ya magonjwa hayo.

Amesema tathmini waliyoifanya imebaini kuwa  watanzania wengi  wana uelewa mdogo kuhusu sheria zao hasa usalama wao mahala pa kazi hivyo kwa kutumia Waandishi wa Habari wanaamini watafikia watu wengi.

Wakili wa OSHA, Rehema Msekwa amesema kila mwajiri katika Taasisi, Kampuni na viwanda anapaswa kujisajili kwani kwa kukaa kimya wanafanya makosa ambayo yanaweza kuwagharimu.

Msekwa amesema kuwa waajiri ambao hawana sera za Usalama na Afya Mahali pa kazi wakibainika wanaweza kutozwa faini ya sh 500,000 ya papo kwa papo.

Mwasilisha mada Mhandishi Shaaban Mbaga amesisitiza kila mtu anao wajibu wa kujilinda na maafa katika vitendea kazi mahala pa kazi.

Mwisho Mkufunzi wa huduma  ya Kwanza Moteswa Meda  amefundisha namna kuweza kumsaidia mtu anapokumbwa na maafa ya moto,kuumwa na nyoka, kumuokoa mtu kwenye majanga ya moto,kupaliwa na chakula kwa wakubwa na wadogo ambapo amewasilisha mada yake kwa vitendo.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa kazi (OSHA), Khadija Mwenda akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu Usalama Mahala pa Kazi. Mafunzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 16, 2024 jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati ya JOWUTA, Tausi Mbowe akizungumza na waandishi wa habari mara baada kufunguliwa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu Usalama Mahala pa Kazi. Mafunzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 16, 2024 jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa JOWUTA, Mussa Juma akizungumza na waandishi wa habari mara baada kufunguliwa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu Usalama Mahala pa Kazi. Mafunzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 16, 2024 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika mafunzo yaliyotolewa na OSHA jijini Dar es Salaam leo Agosti 16, 2024.






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad