Mbunge wa Viti Maalum Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Taifa -UWT (watu wenye ulemavu),Stella Ikupa, leo Agosti 07, 2024 akiwakabidhi wawakilishi wa UWT Kata za Temeke wakati wa kuhitimisha ziara kwa kuwafikia umoja huo wa Wilaya ya Kigamboni na Temeke.
Mbunge wa Viti Maalum Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Taifa -UWT (watu wenye ulemavu),Stella Ikupa, leo Agosti 07, 2024 amekabidhi viti katika wilaya ya Kigamboni na Temeke kwaajili ya kata zao.
MBUNGE wa Viti Maalum Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Taifa -UWT (watu wenye ulemavu),Stella Ikupa, leo Agosti 07, 2024 amehitimisha ziara kwa kuwafikia umoja huo wa Wilaya ya Kigamboni na Temeke.
Akiwa katika Wilaya ya Kigamboni Stela pamoja na mambo mengine amewakabidhi Viti 90 kwaajili ya kata tisa zilizopo katika wilaya hiyo , na alipofika Temeke amekabidhi Viti 230 kwaajili kata zilizopo hapo ikiwa kila kata itapata viti 10.
Akizungumza wakati wa hitimisha ziara hiyo, Mbunge Stela amesema kiasi cha shilingi milioni 18 zimetumika kununua viti ambayo amevigawa katika Wilaya zote za jiji la Dar es Salaam ambapo kila kata za jiji la Dar es Salaam watapata viti 10 ambapo ni sawa na Viti 1020.
Kwa siku ya mwisho, Stela amewaomba UWT na Watanzania kwa ujumla kupinga masuala ya ukatili wa kijinsia kwa watoto, wanawake na watu wenye ulemavu ili jamii kwa ujumla iwe maadili mema.
"Ukatili huu mimi nimekuwa nikiangalia ukatili katika pande zote mbali, ya kiume na ya kike kwa sababu haubagui, Watoto wa kiume na Wakike wamekuwa wakifanyiwa ukatili, wanawake, watu wenye ulemavu, lakini pia tumeona wanaume nao wamekuwa wakifanyiwa ukatili.
Stela ameendelea kuwaomba watanzania kila mmoja aweze kukemea changamoto za ukatili wa kijinsia ili kuweza kupunguza na baadae kumaliza kabisa ingawa hautaisha.
"Turejee kule nyuma tujue watu waliishije basi yale maadili ya miaka ya nyuma pamoja na usasa 'uzungu' ambao tunaenda nao, ingawa kunamambo mazuri yalifanyika huko na ya enzi hizo ambayo tukienda nayo sasahivi yanaweza kuwa msaada mkubwa."
Amesema ni kweli utandawazi upo lakini tukiangalia nyuma Wazee waliishije, waliwezaje lakini kwanini mambo haya hayakuwepo kipindi cha nyuma.. "Naamini yanaweza yatatusaidia na tuaweza kwenda nayo mbele kwa mstakabali wa nchi yetu."
Amesema kuwa tupo vitani kupambana na unyanyasaji wa kijinsia kupitia silaha ya mdomo, kwa kadri ukatili unavyozungumzwa na kuelimisha jamii tunaweza tukashinda vita hiyo ya ukatili.
Katika ziara ya Mbunge Stela, alipokuwa Wilaya ya Ilala alikabidhi viti 360, Kinondoni viti 200, Ubungo viti 140, Kigamboni Viti 90, Temeke Viti 230 huku katika Kituo cha afya cha Kinondoni akikabidhi zawadi za Rais Dkt. Samia za mashuka 20 na Hospitali ya Wilaya ya Ubungo mashuka 21.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kigamboni, Lilian Wasira amemwomba Mbunge Stela kufikisha suala la mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kuharakisha ili waweze kujikwamua kiuchumi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia anavyowaambia wanawake waweze kujikwamua kiuchumi kupitia mikopo.
Pia amezungumzia kuhusiana na mikopo ya halmashauri isiyokuwa na riba pia ameomba ifanyiwe mchakato kwa haraka maana hakuna dalili za kuwepo kwa mikopo hiyo kwa mwaka huu 2024.
"Tulimsikia Rais Dkt. Samia akisema 'Toeni fedha Julai' sasa huu mchakato hauishii.... Naomba na hili ukapambane kwa uwezo wako ili tuweze kujua ni lini fedha hizo zitatolewa na kwa Utaratibu uliopangwa.
Zile pesa zije, ziwanufaishe watanzania ili iwe rahisi mwakani to uchaguzi Mkuu." Amesema
Pia amewaomba wanawake wa UWT, kutoogopa kuchukua mikopo. Pia amewaasa kulipa mikopo ili kuachana na dhana ya kuwa wanawake hawalipi mikopo hiyo.
Kwa Upande wa Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Temeke, Lawama Mikidadi amemshukuru mbunge Stela kwa kuwapa viti hivyo vitakavyosaidia katika mikutano mbalimbali ya Chama.
"Tunamshukuru Mh. Mbunge kwa kutuletea viti 240 kwa maana ya kata 23 kila kata itakuwa imepata viti 10 kwa kweli vinatosha kwa kamati yetu ya utekeleza."
Mbunge wa Viti Maalum Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Taifa -UWT (watu wenye ulemavu),Stella Ikupa, leo Agosti 07, 2024 amehitimisha ziara kwa kuwafikia umoja huo wa Wilaya ya Kigamboni na Temeke.
Baadhi ya UWT wa wilaya ya Temeke wakimsikiliza Mbunge wa Viti Maalum Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Taifa -UWT (watu wenye ulemavu),Stella Ikupa, leo Agosti 07, 2024 jijini Dar es Salaam.
TEMEKE
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kigamboni, Lilian Wasira akimshikuru Mbunge Stela Ikupa kwa Kuwaperekea viti kwaajili ya Ofisi za UWT kata za wilaya ya Kigamboni.
No comments:
Post a Comment