NAIBU waziri wa nishati Mh Judith Kapinga amezindua kituo cah mauzo ya makaa ya mawe kinachoendeshwa na kampuni ya Market insight limited MILCOAL kilichopo katika kijiji cha Paradiso kata ya Ruanda wilaya ya mbinga mkoa wa Ruvuma.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mh Judith Kapinga ambaye ndie mgeni rasmi ameipongeza kampuni ya MILCOAL kwa kuchagua wilaya ya mbinga kwa kufanya uwekezaji kwani kwa kufanya hvo kunasaidia uwekezaji wa uchumi wa ndani ikiwa ni fursa za ajira kwa vijana nchini.
Kufuatia changamoto yakutokuwa na umeme katika mgodi wa MILCOAL, Naibu Waziri Kapinga amesema amezungumza na meneja wa Tanesco Mkoa wa Ruvuma , Eng. Elisius Mhelela, Ambae ameeleza kuwa jitihada zakupeleka umeme bado linaenda ambapo wanatarajia kukamilisha hivi karibuni kwani tayari wameshaanza kufanya kazi na zimebaki taratibu za mwishoni na mradi huo umegharimu Millioni 280 .
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa Ruvuma, Mkuu wa wilaya ya Nyasa Mh Peles Magiri, ametoa shukran kwa kampuni ya MILCOAL kwa kuuchagua mkoa wa Ruvuma kwa kufanya uwekezaji wa makaa ya mawe kwani jambo hilo litarahisisha kupunguza gharama za usafirishaji na ongezeko la fursa za ajira kwa wakazi wa Mbinga na mkoa kwa ujumla huku pongezi kubwa zikienda kwa wizara ya nishati kwa kufanikiwa kuleta umeme katika mkoa wa Ruvuma ambao una vijiji 554 na mpaka sasa vimebaki vijiji viwili pekee kwa mkoa mzima.
Nae mkurugenzi wa mradi MLCOAL amesema wamefanya mauzo ya takriban tani laki tatu na thelathini na kuwepo kwa mgodi huo kutaenda kutoa fursa nyingi za ajira kwa wakazi waishio jirani na maeneo hayo
Kwa upande wa diwani wa kata ya Ruanda Mh Dougras Mwingira ametoa pongezi kwa wamiliki wa Mgodi wa MILCOAL kwani kuwepo kwa mradi huo kumeleta fursa ya wananchi wa kijiji hicho kwa kukuza fursa ya uchumi kwa wakazi wa kata ya Ruanda.
No comments:
Post a Comment