Na Mwandishi wetu
Kilimanjaro. Wakazi wa kijiji cha Makiwaru cha wilaya ya Siha, Sanya Juu, mkoani Kilimanjaro wanasababu ya kutabasamu baada ya kampuni ya michezo ya kubashiri ya betPawa kukamilisha mradi wa kisima cha maji safi.
Mradi huo ulikabidhiwa kwa wanakijiji hao jana na Meneja Masoko wa betPawa Kanda ya Afrika Mashariki, Bi. Borah Ndanyungu ambaye alimkabidhi Bw Eric Salema aliyeomba msaada kupitia mpango wa Dream Maker wa kampuni hiyo.
Bw Salema alituma maombi kupitia kwa kampuni betPawa kupitia mpango wa betPawa Dream Maker ambao unalenga kusaidia watu kutambua ndoto na matarajio yao yenye manufaa kwao na kwa jamii inayowazunguka ikiwa sehemu ya kurudisha kwa jamii.
Akuzungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mradi huo, Bi Ndanyungu alimpongeza Bw Salema (25) kwa kutambua shida ya maji kwa wakazi wa kijiji cha Makiwaru ambao walikuwa wakitembea umabli mrefu kupata huduma hiyo.
Bi Ndanyungu alisema kuwa mradi huu ulichaguliwa kama sehemu ya mpango wa betPawa Dream Maker na kampuni hiyo kutumia Sh milioni 24.4 mpaka kukamilika kwake.
“Bw Salema ambaye ni mkulima na mfugaji, ametambua shida ya jamii na kuwa na ndoto za kutatua tatizo hilo na imefanikiwa. Nampongeza kwa kuwa na moyo wa kusaidia watu na kuleta manufaa kwao,” alisema Ndanyungu.
Alisema kuwa kijiji cha Makiwaru na uhaba wa maji ambao umesababisha mifugo kupotea huku akina mama wasafii umbali mrefu kufuata huduma hiyo, jambo ambalo lilikuwa kero kwao.
"Tunafurahi kwamba alithubutu kutuma ndoto yake na kutambua mustakabali bora wa kijamii na kiuchumi kwa watu wake kupitia upatikanaji wa maji endelevu. betPawa tunajivunia kufanya kazi na Bw Salema kufanikisha mradi huu," alisema Ndanyungu.
Alisema kuwa kisima hicho chenye urefu wa mita 90 kinauwezo wa kuhudumia wakazi 10,000. Mradi huo wa kisima hicho unajumuisha pampu inayotumia umeme ambayo itarahisisha kusambaza maji kwa wakazi wa eneo hilo.
Ndanyungu alisema kuwa mradi wa Makiwaru ulikuwa mojawapo ya ndoto 20 zilizotekelezwa kama sehemu ya msimu wa pili wa mradi wa Dream Maker wa betPawa. Dream Maker ilianzishwa mnamo 2021 na hadi sasa imepokea zaidi ya maombi 15,000.
Kwa upande wake, Bw Salema aliipongeza kampuni ya betPawa kwa kufanikisha mradi huo na kuondoa shida hiyo.
"Wakati mwingine mifugo yetu inakufa kwa kukosa maji. Ikiwa tutapata maji, yatatusaidia kupanda mboga na kufuga mifugo bila matatizo," alisema Salema.
Kwa upande wake, wawakilishi wa kijiji hicho, Bw Mathayo Ngowo na Adela Kimaro waliishukuru kampuni ya betPawa kwa kufanikisha mradi huo na kuwaondolea shida hiyo.
Meneja Masoko wa betPawa Kanda ya Afrika Mashariki, Bi. Borah Ndanyungu wa pili kulia) akimkabidhi ndoo yenye maji mmoja wa wakazi wa kijiji cha Makiwaru cha wilaya ya Siha, Sanya Juu, mkoani Kilimanjaro. Mradi huo umekamilika kupitia mpango wa betPawa Dream Maker ambao ulitokana na maombi yaliyowasilishwa na mkazi wa kijiji hicho Bw Eric Salema.
Wakazi wa kijiji cha Makiwaru cha wilaya ya Siha, Sanya Juu, mkoani Kilimanjaro wakishiriki katika uzinduzi wa mradi huo umekamilika kupitia mpango wa betPawa Dream Maker ambao ulitokana na maombi yaliyowasilishwa na mkazi wa kijiji hicho Bw Eric Salema
Meneja Masoko wa betPawa Kanda ya Afrika Mashariki, Bi. Borah Ndanyungu (wa pili kulia) akikata utepe wa mradi wa maji uliokamilika kwa wakazi wa kijiji cha Makiwaru cha wilaya ya Siha, Sanya Juu, mkoani Kilimanjaro. Mradi huo umekamilika kupitia mpango wa betPawa Dream Maker ambao ulitokana na maombi yaliyowasilishwa na mkazi wa kijiji hicho Bw Eric Salema.
Meneja Masoko wa betPawa Kanda ya Afrika Mashariki, Bi. Borah Ndanyungu (wa pili kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani Sh 24,360,000 kwa Bw Eric Salema (wa tatu kushoto). Bw Salema ndiye aliyewasilisha mpango wa mradi wa maji kwa wakazi wa kijiji cha Makiwaru cha wilaya ya Siha, Sanya Juu, mkoani Kilimanjaro kupitia mpango wa betPawa Dream Maker.
Meneja Masoko wa betPawa Kanda ya Afrika Mashariki, Bi. Borah Ndanyungu akizungumza wakati wa kukabidhi mradi wa maji kwa wakazi wa kijiji cha Makiwaru cha wilaya ya Siha, Sanya Juu, mkoani Kilimanjaro. Mradi huo umekamilika kupitia mpango wa betPawa Dream Maker ambao ulitokana na maombi yaliyowasilishwa na mkazi wa kijiji hicho Bw Eric Salema.
No comments:
Post a Comment