HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 21, 2024

JUMLA YA SHILINGI BILIONI 7 ZIMETOLEWA NA SERIKALI MWAKA 2023/2024 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI WILAYANI NYANG'HWALE


Na Mwandishi wetu,

Mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale Mkoani Geita GRACE KINGALAME amewaomba Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya NYANG'HWALE kwenda katika kata zao na kufanya mikutano ya hadhara na kuwaeleza wananchi mazuri yaliyofanywa na Serikali katika kata zao. Kwa mwaka jana pekee wilaya hiyo ilipokea jumla ya shilingi BILIONI SABA kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mkuu wa wilaya ya NYANG'HWALE GRACE KINGALAME amesema hayo wakati wa kikao cha baraza la madiwani Mkutano wa Nne wa Baraza la Madiwani kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na amesema wasifanye mikutano ya kutatua kero pekee lakini na kuyaeleza mazuri yaliyofanywa na serikali.

KINGALAME akasisitiza katika kuelekea kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa wananchi wakipata taarifa sahihi za miradi iliyotekelezwa na serikali diwani utaendelea kuaminika katika nafasi yako kwa wananchi, mbunge pamoja na Rais SAMIA SULUHU HASSAN wataendelea kuaminika kwa sababu ya kuzungumza na kuelezea mema yaliyotekelezwa na serikali ya awamu ya Sita.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya NYANG'HWALE JOHN ISSACK amesema wilaya hiyo inazidi kusonga mbele katika usimamizi wa miradi ya afya na elimu kutokana na ushirikiano anaoupata kuanzia kwa kamati ya Ulinzi na usalama ya wilaya hiyo ikiongozwa na Mkuu wa wilaya GRACE KINGALAME na wakuu wa idara na vitengo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji HUSNA TONI bila kushahaulika watendaji wa kata na vijiji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad