HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, August 10, 2024

FAIDA FUND YAVUKA MALENGO KWA MWAKA MMOJA

 

Meneja wa Mfuko wa Faida Fund kushoto Fred Msemwa akimsalimiana na Hemedi Masumai Mwakilishi wa Msimamizi wa mfuko huo (CRDB ) wakati wa Mkutano mkuu wa kwanza wa mwaka wa wawekezaji wa mfuko Faida Fund uliofanyika leo Agosti 10,2024 katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere. Anayeshuhudia katikati yao ni  ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo Abdul Razaq Badru.

Naibu Katibu Mkuu Utumishi,  Xavier Daudi akiwasilimia wanachama wa Mfuko wa Faida Fund katika Mkutano Mkuu wa mwanzo wa Mwaka uliofanyika leo Agosti 10,2024  Jijini Dar es Salaam

Naibu Katibu Mkuu  Utumishi Xavier Daudi , kushoto Abdul Razaq Badru Mwenyekiti wa Bodi ya Faida Fund, kulia Hemedi Masumai, na Mwakilishi wa Msimamizi wa Mfuko wa Faida Fund (CRDB) wakiwa katika Mkutano Mkuu wa kwanza wa Mwaka wa wawekezaji wa mfuko huo uliofanyika leo Agosti 10, 2024  jijini Dar es Salaam

Wananchama wa Mfuko wa Faida Fund wakifuatilia mada  mbalimbali wakati wa mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa mfuko huo uliofanyika leo Agosti 10,2024 jijini Dar es Salaam


Na Karama Kenyunko Michuzi Tv 
MFUKO wa uwekezaji wa Faida Fund kwa kipindi cha Mwaka mmoja umevuka malengo ambayo uliwaahidi wanachama wake ya kuwa mfuko utakuwa na faida asilimia 9.7 hatimaye imepitiliza lengo hilo na kufikia asilimia 12 ya faida.

Hayo yameelezwa na Meneja wa Faida Fund Fred Msemwa, leo Agosti 10 2024 katika Mkutano Mkuu wa kwanza wa mfuko huo uliohudhuriawa  na idadi ya zaidi ya asilimia 80 wanachama wake.

"Wakati tunaanza mwaka jana tulitoa ahadi kwa wawekezaji kuwa mfuko utakuwa na faida isiyopungua asilimia 9.7  lakini  Kutokana na juhudu na usimamizi imara na umakini wa Meneja Faida Fund (Watumishi Housing Investment) lakini tumefikia zaidi ya tuliyoahidi kesi yetu imefikia faidia ya asilimia 12", amesema Msemwa.

Amesema pamoja na kuwa na gharama za kuanzia mfuko lakini bado mfuko huo ulipata faida kwa kasi.

Amesema kuwa mfuko huo umepata faida haraka haraka kwa sababu ya matumizi ya Teknolojia na kuungwa mkono na wadau pamoja na serikali.

Amesema kuwa matumizi ya mfumo wa malipo ya serikali umeufanya mfuko huo uwe na uhakika , usalama na haraka kwenye ufanyaji wa miamala.

"Huu ndio mfuko pekee wenye kutumia mfumo wa GePG ambao unawezesha kasi ya ufanyaji miamala .Hatuna mfuko ambao unawekeza leo halafu unapata faida lakini Faida Fund unapata faida leo leo".

"Hili jambo kubwa kuwepo kwa soko hili , wawekezaji wanaweza kukuwa kwa kasi zaidi kwa sababu ya miamala ya kasi ukiwekeza mifuko mingine mathalan ukiwekeza ijumaa ukapata vipande Jumanne umekosa faida kwa siku nne." amesemwa Msemwa.

Msemwa amesema kuwa licha ya soko la uwekezaji wa vipande kukosa ushindani kwa sababu ya changamoto ya Watanzania wachache kuwekeza lakini mfuko huo unatoa faida shindani kwa sababu wawekezaji wachache walikuwepo wanatoa faida shindani.

Amesem kuwa mfuko huo unatoa fursa kwa wawekezaji wadogo kushiriki kwa sababu unaweza kuanza kuwekeza kwa shilingi 10000.
 
Msemwa amesema kuwa Mfuko huo umepanua wigo wake kwa kuwafikia mpaka wananchi wa vijijini .

"Tumeongeza upatikanaji wa huduma jumuishi za fedha katika maeneo ya vijijini watu wanaweza kujiunga na mfuko na kuwekeza..kupitia simu za vitochi" amesema Msemwa.

Tumeimarisha mifumo salama ya kifedha mfumo wa GEpG.
Amesema kuwa bidhaa nyingine ya Faida Fund ni uwekezaji kwa ajili ya mtoto kwa ajili ya kujisomesha elimu yake ya juu mpaka anamaliza kupitia akiba yake.

Abdul Razaq Badru mwenyekiti wa bodi ya Faida Fund  amesema kuwa maendeleo ya mfuko huo ni mazuri .

"Mfuko wa  uwekezaji wa Faida Fund kwa mwaka mmoja imeongeza faida ya shilingi 25.6 Bilioni kufikia mwezi Juni mwaka huu ambapo ulianza na shilingi 15.6 Bilioni mwaka jana mwezi juni" 

Amesemaa kuwa wawekezaji wameongozeka  kutoka 2041 mwaka jana na kufikia  4806 ongezeko la asilimia 60 . 

Hemed Masumai Mwakili wa Benki ya CRDB ambayo ndio msimamizi wa mfuko huo amesema kuwa mfuko upo salama .
  
"CRDB tukiwa wasimamizi wa mfuko jukumu letu kufanya uangalizi wa mali za mfuko kuhakikisha zipo salama, kuhakikisha viwango vya uwekezaji vinazingatiwa"

"Tunawathibitishia kwamba shughuli za uwendeshaji zimetekelezwa kuzingatia kulinda wawezaji" amesema 

Amesema kuwa Mfuko wa Faida fund umefuata utaratibu wote kama ambavyo tulikubaliana kwenye waraka wetu.

Mkaguzi wa Hesabu wa mfuko huo Pamak Associates wakitoa taarifa za ukaguzi wa mfuko huo amesema kuwa Muhtasari wa fedha unaendana na taarifa za fedha zilizokaguliwa kwa kutumia viwango vya bodi ya ukaguzi ya kimataifa (IFRS ) ukaguzi uliopewa namna ya ISo 810.

Meshark Mafeko mmoja wa wawekezaji katika mfuko hui ametoa ushuhuda wake baada kuwekeza na kupata faida.

Mafeko amesema kuwa hakuwa na shaka na mfuko huo kutokana na mifumo yake 'nilipoona mfuko malipo yake ni ya mfumo wa serikali kisha mfuko upo chini ya serikali".

Amesema kuwa baada kujiridhisha mfuko huo unatija aliwaanzisha kikundi cha wajasiriamali alicholenga kuwainua wanawake kiuchumi kinachoitwa 'Bint Mwenye Ndoto'.

Elizabeth Malco mtumishi wa Serikali anayefanya kazi wilayani Korogwe Mkoa wa Tanga amejifunza uwekezaji kupitia vipindi vya televisheni baadaye akazidi kuelewa instragram ndipo alipoonza kuwekeza na kwamba mfuko huo unafaida za wazi.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad