* Wawekezaji Faida Fund juu takriban 60%!
* Faida, Thamani, Ukubwa wa Mfuko Vyapaa!
* Faida Kuongezeka, Mifumo Kuboreshwa!
(Aishukuru Serikali, Wadau kwa Mafanikio.
Na Derek Murusuri, Royal Publishers, Dar es Salaam 13 Agosti, 2024
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wawekezaji wa Mfuko wa Faida (Faida Fund), Bw. Abdul-Razak Badru, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuboresha mazingira ya biashara nchini, hadi Bodi yake kupata Mafanikio makubwa.
“Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali kwa ujumla kwa kuendelea kusimamia na kuweka mazingira bora ya biashara nchini,” alisema.
Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania
Bwana Badru, ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), alibainisha kuwa Faida Fund imepata ongezeko kubwa la idadi ya wawekezaji, ikiwa ni pamoja na
kuongezeka kwa thamani ya Mfuko, kutokana na kuboreshwa kwa mazingira ya kufanya biashara nchini.
“Kwa kipindi kilichoishia Juni, 2024, idadi ya wawekezaji ilikua na kufikia 4,806 sawa na ongezeko la asilimia 58 la Wawekezaji waliojiunga katika Mfuko, ukilinganisha na kipindi kilichoishia tarehe 30 Juni, 2023 ambapo idadi ya wawekezaji ilifikia 2,041,” alisema Bw. Badru.
Mwenyekiti huyo alikuwa akiwasilisha taarifa yake ya mwaka ulioishia Juni, 2024, kwenye Mkutano Mkuu wa kwanza wa Wawekezaji wa Mfuko wa Faida (Faida Fund), uliofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
“Kwa kipindi kilichoishia Juni, 2024, idadi ya wawekezaji ilikua na kufikia 4,806 sawa na ongezeko la asilimia 58 la Wawekezaji waliojiunga katika Mfuko, ukilinganisha na kipindi kilichoishia tarehe 30 Juni, 2023 ambapo idadi ya wawekezaji ilifikia 2,041.”
Faida kwa Wawekezaji ilikuwa kubwa ikilinganishwa na kigezo linganifu (performance Benckmark). Kwa
kipindi cha miezi nane (8) ya mwanzo kilichoishia 20 Juni, 2023, faida iliyopatikana ilikuwa asilimia
10.0 na imeendelea kuongezeka hadi kufikia asilimia 12 kwa kipindi kilichoishia 30 Juni, 2024.
Mafanikio mengine makubwa ya kujivunia kwa uongozi mahiri wa mfuko, ni kuongezeka kwa thamani halisi ya mfuko, kutoka 15.6bil./- Juni 2023 hadi 25.6 bil./- kufikia Juni,
2024.
Bw. Abdul-Razak Badru
Mwenyekiti huyo pia alibainisha kuwa, ongezeko la thamani ya Mfuko limetokana na faida nzuri iliyopatikana, matumizi ya teknolojia katika miamala ya uwekezaji, kuongezeka kwa imani na mafanikio ya elimu juu ya faida zinazopatikana kupitia Mifuko ya uwekezaji wa pamoja.
Masoko ya Fedha
Kwenye maendeleo ya Soko la Mitaji na Dhamana, Bw. Badru alisema kumekuwepo na maendeleo
mazuri na kuongeza kuwa, “katika kipindi kilichoishia 30 Juni, 2023, kumekuwa na ongezeko la asilimia 4.1.
Utendaji wake hupimwa kwa kuangalia mabadiliko ya Fahirisi (Tanzania Share Index).
Watumishi Housing Investments (WHI) imepata mafanikio makubwa zaidi ya ilivyotarajiwa katika kipindi kilichoishia Juni, 2023. Mafanikio hayo ni pamoja na kuanzisha Mfuko wa Faida, ambao unatoa pato shindani katika soko. Wadau wa masoko ya fedha wamesema kuwa haya ni mafanikio makubwa katika sekta ya fedha, yanayochangia katika uthabiti wa uchumi nchini.
“Bwana Badru, ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), alibainisha kuwa Faida Fund imepata ongezeko kubwa la idadi ya wawekezaji, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa thamani ya Mfuko, kutokana na kuboreshwa kwa mazingira ya kufanya biashara nchini.”
Naye Bw. Abdulmajid Nsekela, Mwangalizi wa Mfuko huo wa Faida kwa Wawekezaji, amewashukuru wanachama kwa imani yao kwa Benki ya CRDB na kwamba maslahi ya wenye vipande ndani ya Mfuko wa Faida, yanalindwa.
Bw. Nsekela ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, alisema kuwa majukumu yake ni uangalizi wa mali za mfuko, kukokotoa mahesabu ya thamani ya mfuko na kuhakikisha viwango vya uwekezaji vinazingatiwa.
Taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG, Bw. Charles Kichere, ililidhishwa na muhtasari wa hesabu za Mfuko wa Faida.
Bw. Abdulmajid M. Nsekela Meneja wa Mfuko wa Faida, Dkt. Fred Msemwa, amesena kuwa Mfuko wa Faida ulianzishwa Novemba 2022 na kuanza rasmi mauzo ya vipande
tarehe 1 Januari, 2023. Huu ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja, ambao
hutoa fursa kwa Taasisi na watu binafsi kuwekeza kipato chao cha ziada kwa kipindi kifupi cha kati au muda mrefu kwa faida na ukwasi madhubuti.
Dkt. Msemwa ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Watumishi Housing Investments (WHI), ameelezea faida za kuwekeza katika Mfuko wa Faida na Amana za Mabenki kuwa ni pamoja na wawekezaji wake kuuza vipande vyao wakati wowote (baada ya siku 90 tangu kuanza kuwekeza).
“...faida nyingine ni kuwa hakuna gharama wakati wa kuingia au kutoka
katika uwekezaji wetu na pia mapato ya uwekezaji hayatozwi kodi ya zuio,” alisema Dkt. Msemwa.
Faida nyingine ni kuwa uwekezaji katika Mfuko wa Faida hauna muda maalum au ukomo, mwekezaji anaweza kutumia vipande alivyowekeza kwenye Mfuko kama dhamana ya kupata mkopo benki na pia Mfuko unatoa suluhisho kwa makundi maalum kama vile wastaafu, Watoto na Wawekezaji wa pamoja.
“Faida nyingine ni kuwa uwekezaji katika Mfuko wa Faida hauna muda maalum au ukomo, mwekezaji anaweza kutumia vipande alivyowekeza kwenye Mfuko kama dhamana ya kupata mkopo benki…”
Dkt. Fred Msemwa
Awali, Bw. Badru aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Wengine aliowashukuru ni Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, Msimamizi wa Mfuko (CRDB), Soko la Hisa la Dar es Salaam, Madalali wake, Wajumbe wa Bodi ya Mfuko, Wafanyakazi na Wadau wote.
No comments:
Post a Comment