HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, July 7, 2024

TIA yajiwekea mpango mkakati wa Kuendeleza vijana wenye Ubunifu

 

Wanafunzi wakipata maelezo katika Banda la TIA kwenye Maonesho ya 48 Biashara Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.


*Ni pamoja na kuwaunganisha katika soko la ajira kwa kurasimisha kibiashara

Na Mwandishi Wetu TAASISI ya Uhasibu Tanzania (TIA) imesema kuwa katika vijana wanaosoma katika Taasisi hiyo wakawa na ubunifu watasimamiwa katika matokeo chanya ya bunifu zao.

Hayo ameyasema Mkuu wa Sehemu Ukuzaji na Uendelezaji wa Wanafunzi Kitaaluma na Kitaalam wa TIA Imani Matonya katika Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa Taasisi hiyo imekuwa inasimama bega kwa bega na wanafunzi wenye ubunifu ikwa ni lengo la kufanya vijana waweze kukua na pindi wanapohitimu wanakwenda kufanyia kazi ikiwa kwao ndio sehemu ya ajira.

Amesema kuwa katika majukumu ya Taasisi kwa wabunifu wanawarasimisha kwa kusajili kampuni pamoja na kuwapa wanasheria ili waweze kuendesha kampuni hizo kisheria.

Matonya amesema katika mawazo ya ubunifu hadi sasa zaidi mawazo yenye 100 yameingia sokoni ambapo nia ajira zaidi ya watu 500.

Amesema mwanafunzi Kigoma amebuni kifaa cha kakaushia Samaki kwa kutumia mwanga wa jua ambapo kifaa hicho kinaweza kutumika katika kipindi cha masika na wakati huo huo kinaweza kukausha mboga za majani.

Amesema kuwa katika bunifu na mawazo Taasisi inasimamia kwa ajili ya ulezi katika eneo la utaalam kwa kukutanishwa na wataalam wabobezi katika maeneo waliosomea

Amesema kukutanishwa na wataalam wabobezi kuhakikisha wanaendelezwa ili wasizitelekeze bunifu hizo ambazo zinakwenda kutoa suluhisho katika jamii.

Amesema katika majukumu ya ulezi wa Taasisi kwa vijana ambao wamekuwa na ubunifu ni pamoja na kuwaunganisha katika soko la ajira kwa kurasimisha biashara zao.

Mwanafunzi wa Mwaka wa Kwanza Henock William amesema kuwa katika Ubunifu wake umejikita katika uandishi na Usalama wa Wananchi ambapo mfumo unakwenda kuleta mapinduzi kwa njia simu na komputa.

Amesema amesema kuwa amesema mfumo huo unafanya mtu kuandika na kupata mtiririko mzuri ikiwemo kuandika wasifu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad