HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 10, 2024

TANZANIA KUNUFAIKA NA MRADI WA ‘SUSTAINABLE OCEAN PHASE II’

 

TANZANIA ni miongoni mwa nchi zitakazo nufaika na mradi wa “Sustainable Ocean Phase II"unaosimamiwa na Taasisi ya Kitaifa ya Haki za Binadamu nchini Denmark(Danish Institute of Human Rights).

Hayo yamebainishwa na Mshauri Mkuu wa Taasisi hiyo Bi.Carol Rask wakati walipotembelea Ofisi ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora hivi karibuni Jijini Dodoma.

Bi.Carol alisema mradi huo unaotarajiwa kutaekelezwa kwa muda wa miaka minne unafadhiliwa na SIDA.

“mradi huo umelenga kuimarisha ulinzi wa mazingira kwa wavuvi wadogo na jamii zinazowazunguka”alisema Bi.Carol

Aidha Bi Carol alisema katika kutekeleza mradi huo wamefanya ziara nchini Tanzania iliyolenga kutafuta wadau mbalimbali ambapo moja ya wadau hao ni Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Bi Carol alisema wametembelea Tanzania ili kujifunza zaidi kuhusu maeneo yanayoweza kuzingatiwa ili kutekeleza mradi huo ikiwemo kukutana na Wadau mbalimbali ili kupata maoni yao pamoja na kuhakikisha watendaji wa Serikali na Sekta binafsi wanachukua hatua za kuimarisha haki za binadamu kwa wavuvi wadogo na jamii inayowazunguka kwa kuzingatia sheria za kitaifa,Sera na mipango inayohusiana na utawala wa wavuvi.

Naye,Mratibu Miradi Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi.Jovina Muchunguzi alisema kuwa Tume inaendelea na mchakato wa uwandaaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu na Biashara kwa kushirikiana na wadau kutoka Serikalini na Sekta binafsi .

"Tume imeshakutana na wadau hao na kuwaeleza hatua mbalimbali zilizofanyika za uandaaji wa mpango kazi huo"alisema Bi.Jovina

Aidha ,Bi Jovina alisema kuwa Tume,katika mchakato wa uandaaji wa Mpango kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu na Biashara eneo moja la kipaumbele ni kilimo na uchumi wa bluu ndani yake kuna shughuli za uvuvi.

"Eneo hili ni muhimu katika maisha ya watanzania na katika mpango unaondaliwa"alisema Bi.Jovina

Kwa hatua nyingine ujumbe huo ulieleza kuwa ipo tayari kushirikiana na Tume katika masuala ya Mafunzo,Tafiti,Kuandaa miongozo ya kusimamia haki za binadamu na masuala mengine.

Ugeni huo ulipokelewa na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe.Mohamed Khamis Hamad,Katibu Mtendaji Bwa.Patience Ntwina na baadaye mazungumzo hayo kuongozwa na Bi. Jovina Muchunguzi pamoja na Bw.Constatine Mugusi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad