HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 3, 2024

WAZIRI SORAGA AZINDUA MRADI WA AZURE AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI ZANZIBAR


MRADI wa Nyumba za Kifahari kwa ajili ya Watalii (AZURE) wenye bilioni 24 wazinduliwa rasmi Visiwani Unguja Wawekezaji wawekewa Mazingira rafiki kwa Uwekezaji wenye Tija kwa Lengo la Kutangaza Utalii Visiwani humo.

Akizungumza na Wanahabari Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mudrick Ramadhan Soraga amesema Mradi huo wa Makazi ya kifahari (AZURE) itaenda kuwa kielelezo tosha kuwa Uwekezaji visiwani Zanzibar kwa wageni inawezekana na milango ipo wazi kwa wazawa na wageni.

Aidha amesema pia italeta muamko kwa wawekezaji binafsi ikishirikiana na Makampuni mbalimbali kuja kuwekeza Visiwani Zanzibar na milango ipo wazi kwa kupokea wageni kwa uwekezaji.

Hata ameongeza kuwa Wizara hiyo imeitikia wito kwa Viongozi wa Kitaifa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Hussein Mwinyi kwa pamoja wamekuwa wakikaribisha wawekezaji nchini Tanzania hivyo nakuhaidi kuwa wataendelea na spidi hiyo hiyo na wapo tayari kuwapokea na kuonesha ushirikiano.

Aidha Soraga amefafanua zaidi kuwa Mradi huo wa "Azure" utawanufaisha Wazanzibari pamoja na Wawekezaji wenyewe katika kutangaza Utalii na Kuimarisha na kuongeza pato la taifa kwa kupitia watalii.

"Wenzetu wanakuja kuwekeza kwa dhamira ya kutafuta faida vilevile kwa kuvutiwa na Mazingira yaliyomo Kusini unguja . "

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Mahamoud amesema Mradi huo una thamani ya wastani wa dola za Kimarekani Milioni 10 sawa na Bilioni 24 Shilingi za kitanzani hivyo wanatambua kuwa wawekezaji hao wanapata faida katika shughuli zao za utalii

"Nasisi wanakusini kwakuwa wenzetu wako mbali tutawakimbiza kwa kuhakikisha tunashirikiana na wawekezaji kutoka nje na makampuni i ya Utalii ili kusaidia vivutio vya utalii kukua na kuongezeka idadi ya Watalii kutoka wa kiamataifa"amesema.

Aidha hatuna ni budi kutambua kuwa Wewwkezaji hao wamekuja kutafuta faida ila wapo wenzetu ambao hawajaweza na kuwa na uelewa hivyo tufahamu kuwa muda wa kuchezewa haupo na niwafahamishe muwekezaji anadhamira nzuri ya kuwekeza Moli ya kisasa na itakuwa ya kwanza na yupo katika mazungumzo hivyo tutaendelea kumuunga mkono na kumuhakikishia Usalama.

Nae Mkurugenzi wa Kampuni ya "The Village Group " Simon Nikita ameeleza kuvutiwa kwake na uwekezaji huo visiwani humo ni kutokana na kuwa Zanzibar, inayojulikana kwa fukwe zake za asili, urithi tajiri wa kitamaduni, na mandhari ya kupendeza, sasa ndio sababu inayokwenda kushuhudia maendeleo makubwa katika sekta ya mali isiyohamishika.

Nikita ameeleza kuwa unaweza kununua villa yako ya kifahari ya hali ya juu, kisha una uhakika wa 100% juu ya Kurudi kwa Uwekezaji, Faida na Umiliki wa Uwekezaji huo.

Pia amewatoa hofu Serikali kuwa waweke imani juu ya Maendeleo hayo kwani swala la uwekezaji huo wa ujenzi wa nyumba za kifahari linawezekana na linaweza kufanywa na Kampuni ya The Village Group ya Zanzibar kwa mradi wa "AZURE" ambao unalenga kuleta umiliki wa Majumba ya Kifahari kwa yeyote anayependa.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mudrick Ramadhan Soraga kushoto kwake Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja,Kulia kwake Mkurugenzi wa Kampuni ya Uwekezaji "The Village Group Simon Nikitas pichani wakiwa na Chepe kuashiria kuanza kwa Mradi wa ujenzi wa Nyumba za Kifahari ( AZURE) utakaowanufaisha Wazanzibari pamoja na Wawekezaji wenyewe kutoka Kampuni ya "The Village Group
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mudrick Ramadhan Soraga akizungumza machache mara baada ya kuzindua Mradi mpya wa ujenzi wa nyumba za kifahari wa (AZURE) Visiwani kwa lengo la kuwapa Mazingira rafiki kwa watalii wanaoingia Visiwani Zanzibar kwa kupata sehemu salama
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mudrick Ramadhan Soraga kushoto kwake Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja,Kulia kwake Mkurugenzi wa Kampuni ya Uwekezaji "The Village Group Simon Nikitas pichani mara baada ya kuzindua mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Kifahari (AZURE) wenye thamani ya shilingi za Kitanzania Bilioni 24 ambao utajengwa Unguja Visiwani Zanzibar

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad