HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 11, 2024

WANAWAKE WATEGEMEWA ELIMU KUBORESHA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

 

Mwenyekiti wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Rufaa, Mbarouku Salim Mbarouku akizungumza wakati akifungua Mafunzo kwa Wawakilishi wa wanawake katika mafunzo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Juni 11, 2024.
Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Bi. Giveness Aswile akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo kwa Wawakilishi wa wanawake katika mafunzo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Juni 11, 2024.





Baadhi ya Wawakilishi wa Wanawake wakiwa katika 
ufunguzi wa Mafunzo kwa Wawakilishi wa wanawake katika mafunzo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Juni 11, 2024.

Picha ya pamoja.

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
KUELEKEA uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025 Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewaomba Wawakilishi wa Wanawake kutoa elimu kwa Wanawake wengi zaidi ili wajitokeze kujiandikisha katika daftari la kudumu la Mpiga kura.

Hayo ameyasema leo Juni 11, 2024 Mwenyekiti wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Rufaa, Mbarouku Salim Mbarouku wakati akifungua Mafunzo kwa Wawakilishi wa wanawake katika mafunzo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Amesema INEC inathamini Mchango wa Wanawake katika ushirikiano wao wa mara kwa mara hususani wakati wa michakato ya uchaguzi nchini.

“Lengo la kukutana hapa ni kupeana taarifa kuhusiana na maandalizi ya zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura pamoja na masuala mengine ikiwemo uhakiki wa vituo vya kuandikisha wapiga kura, uboreshaji wa majaribio, ushirikishwaji wa wadau mbalimbali kama tufanyavyo hapa pamoja na ununuzi wa vifaa… Wanawake mnanafasi kubwa ya kufikia jamii tunaomba ujumbe na hamasa hii iwafikie wananchi kwa wakati na usahihi kupitia majukwaa yenu.” Ameeleza.

Jaji Mbarouku amesema Maboresho hayo ya daftari la kudumu la Mpigakura litahusisha Wale waliotimiza Miaka 18, Wale watakaotimiza Miaka 18 mwaka 2025 na wale ambao wamezidi umri na hawakujiandikisha na kuwaondoa wale waliopoteza sifa.

Pia amesema tume inatarajia kupata ushirikiano mkubwa zaidi kutoka kwa Wanawake kwani wanauwezo wa kuwafikishia wananchi taarifa sahihi na kwa wakati juu ya taarifa zinazohusu zoezi lililopo mbele la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kuwahamasisha wananchi kujiandikisha ili wawe wapiga kura.

Jaji Mbarouku amesema, katika maboresho hayo ya daftari,tume imewapa kipaumbele maalumu Wanawake ili waweze kushiriki kikamilifu kufanya maboresho ya taarifa zao na kujiandikisha.

Licha ya hayo Jaji Mbarouku amesema kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuzindua rasmi zoezi la maboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Kigoma Julai Mosi 2024.

INEC imewaomba Wananchi kutumia Muda utakaopangwa vizuri ili kuondokana na siku za mwisho kuwa na watu wengi zaidi na siku za mwanzo kuwa na watu wachache wakati wa kujiandikisha.

Aidha Jaji Mbarouku amesema kuwa tayari wameshafanya majaribio ya Vifaa vya kuandikishia kwaajili ya maboresho ya daftari la kudumu la mpiga kura na  kueleza kuwa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2024/2025 umeboreshwa zaidi kwa kutumia teknolojia ya BVR (Biometric Voter’s Registration) ya kisasa zaidi kwa kuwekwa programu endishi na hiyo ni pamoja na kupunguzwa uzito kwa vifaa na kubebeka kiurahisi hali itakayorahisisha kazi kwa watendaji katika maeneo mbalimbali hususani maeneo ya vijijiji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad