HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 29, 2024

TUCASA WAASWA KUWA NA WIVU WALIZOZICHAGUA

 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akizungumza na Chama cha Umoja wa Mandarasi Tanzania (TUCASA) wakati wa kongamano lililofanyika Juni 27 na 28, 2024 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko ametoa wito kwa Chama cha Umoja wa Mandarasi Tanzania (TUCASA) kuona wivu kwa kazi walizochagua kuzifanya na kuachana na Rushwa pamoja na ujasiliamali tenda.

Serikali kupitia Takukuru itaendelea kuchukua hatua za kisheria kwa watumishi wanaojihusisha na matendo ya rushwa.

Hayo ameyasema Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Biteko akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan rasmi wakati wa kufunga kongamano la Chama cha Umoja wa Mandarasi Tanzania (TUCASA), lililofanyika Juni 27, 28, 2024 katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam (JINCC).

"Jambo la Rushwa si jambo la Taassi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ni jambo la mitazamo yetu anayetoa na anayepokea."

Pia amewaomba watendaji Serikalini wajenge taswira chanya kwa wakandarasi na watoa huduma wa Tanzania.

Akizungumzia hoja ya Makandarasi kutokulipwa kwa wakati, Dkt. Biteko amesema kuwa Serikali imeshaanda mpango wa kuhakikisha makandarasi wazawa kupewa kipaumbele katika malipo ya kazi wanayofanya.

“Kama kunamtanzania anauwezo wa kufanya kazi fulani apewe aifanye, tumsimamie, tumkuze tumfanye kiwa mwenye uwezo, kesho atakuwa mlipakodi mkubwa, tuone heshima kuwapa kazi watanzania tuone heshima tukiwaona watanzania wanafanya kazi nyingine nchi nyingine."

Rais samia anawapenda Makandarasi anataka kuona utajiri unakuwa mikononi mwenu... Anataka nyinyi mchangamkie fursa ya kazi hizo nyinyi tendeni kwa haki " Amesema

Pia Dkt. Biteko amesema kunampango wa Makandarasi wa ndani kuwekwa kwenye kipaumbele cha kuahakikisha miradi yote inatekelezwa kwa fedha za mikopo kutoka kwa wadau wa maendeleo kutengwa kwa asilimia isiyopungua 20 kwa ajili ya makandarasi wa ndani.

Licha ya hayo Dkt. Biteko amewapongeza wakandarasi wanawae kwakuamua kufanya kazi za Makandarasi pia amewaasa kuongezeka zaidi kwani wao ni waaminifu ukilinganisha na Makandarasi Wanaume

"Niwaombe Wanawake ongezeni bidii na nyinyi muweze kushindana…..Serikali ipo tayari wakati wowote kusikiliza wapi hamnufaiki na Mandarasi wazawa ‘Local content’." Amesema

Akitoa maagizo ya Rais Samia Dkt. Biteko amesema wahahakikishe Makandarasi wa ndani wanatekelezwa ipasavyo kwa vitendo miradi wanayopewa.

Serikali tayari wameshakamilisha mpango wake kwa Makandarasi Wanawake katika Mwaka wa fedha wa 2024/2025 wizara imetenga miradi ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 120 za lami ambazo zitashindanishwa kwa makandarasi wa ndani peke yao.

Amesema katika kilomita hizo 120 hawajawasahau makandarasi Wanawake, zimetengwa kilomita 20 ambazo zitashindanishwa kwa Makandarasi Wanawake tuu.

Ameeleza kuwa wakati wa kuzitangaza tenda za kilomita hizo 20 hawatatangaza kwa kutumia mtandao mmoja bali watakagwa katika kilomita tano tano ili Wakandarasi Wanawake wenye kampuni za Ukandarasi waanzie hapo.

Mkutano huo umefanyika kwa siku mbili na kuhudhuliwa na Makandarasi na wadau wengine zaidi ya 2000.

Kauli mbiu katika Kongamano la TUCASA kwa Mwaka huu ni; Mjenga Nchi ni Mwananchi, Makandarasi Wazawa Tunaweza.




Baadhi ya Washiriki wakiwa katika kongamano la Makandarasi wazawa hapa nchini

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad