HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 8, 2024

TAREA YAOMBA UWAKILISHI WA REA, MAPITIO YA SERA YA NISHATI


Kamishina wa Umeme na Nishati Jadidifu Tanzania, Mhandisi Innocent Luoga akitoa hotuba ya Uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nishati Jadidifu  (REW) Mwaka 2024. Kushoto kwake ni Meneja Mafunzo wa sun king – Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa REW, Immaculate Shija na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wadau wa Nishati Jadiditu Tanzania (TAREA), Mhandisi Prosper Magali.

Kamishina wa Umeme na Nishati Jadidifu Tanzania, Mhandisi Innocent Luoga akitembelea mabanda mbalimbali ya washiriki wa Maadhimisho ya Wiki ya Nishati Jadidifu  (REW) Mwaka 2024.


Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya REX ENERGY, Mhandisi Francis Kibhisa (kushoto) akimweleza Kamishina wa Umeme na Nishati Jadidifu Tanzania, Mhandisi Innocent Luoga  (wa pili kulia_ shughuli na ufanisi wa kampuni yake katika huduma za nishati jadidifu Tanzania katika Maadhimidho hayo ya Wikiya Nishati Jadidifu. Kulia ni Katibu Mtendaji wa TAREA, Mhandisi Mathew Matimbwi.

Mratibu wa Miradi wa kampuni ya REX ENERGY, Motatiro Kibhisa akizungumza na wageni waliotembelea banda la kampuni hiyo katika maadhimisho ya Wiki ya Nishati Jadidifu 2024 mkoani Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa REX ENERGY, Mhandisi Francis Kibhisa.

Ofisa Rasilimali katika Jumuiya ya Wadau wa Nishati Jadidifu Tanzania (TAREA), Suzana Machange akimweleza Kamishina wa Umeme na Nishati Jadidifu Tanzania, Mhandisi Innocent Luoga shughuli za TAREA nchini.

JUMUIYA ya Wadau wa Nishati Jadidifu Tanzania (TAREA) imeiomba serikali kupitia Wizara ya Nishati kufikiria kupitia upya Sera ya Nishati ili kuwezesha kutilia mkazo matumizi ya nishati mbadala kwa aina zote za matumizi.

Aidha, TAREA imeiomba Wizara ya Nishati kuishauri Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuteua mwakilishi wa sekta binafsi katika Bodi ya REA kutoka kwa miongoni mwa wadau wa nishati jadidifu.

Katibu Mtendaji wa TAREA, Mhandisi Mathew Matimbwi alibainisha hayo alipokuwa wakati akimkaribisha Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Tanzania, Mhandisi Innocent Luoga katika ufunguzi rasmi wa Wiki ya Kitaifa ya Nishati Jadidifu 2024 inayomalizika leo, Dar es Salaam.

Luoga alikuwa akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felichesmi Mramba.

Kwa mujibu wa Matimbwi, TAREA inaunga mkono azma inayoendelea ya kuwezesha upishi safi kupitia uhamasishaji wa matumizi ya teknolojia ya nishati mbadala kwa kupikia itakayochangia uhifadhi wa misitu ya Tanzania, kuboresha utunzaji wa mazingira na kupunguza ongezeko la hewa ukaa.

 "Tunaiomba serikali iangalie upya Sera ya Nishati ili iweze kusisitiza matumizi ya nishati mbadala kwa aina nyingine zote za matumizi badala ya kuzingatia uzalishaji wa umeme pekee." Alisema Matimbwi na kuongeza kuwa TAREA inaishukuru serikali kwa kuzindua Mkakati wa Upikaji Safi na mwogozo unaotaka kuwepo kwa ufumbuzi wa matumizi ya nishati.

Kwa mujibu wa Matimbwi, TAREA inaiomba Wizara ya Nishati kuishauri Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuteua mwakilishi wa sekta binafsi katika Bodi ya REA kutoka kwa wadau wa nishati.

"Kuna mitandao kadhaa ya nishati ambayo mwakilishi anaweza kuteuliwa. Kama ilivyo sasa, wahusika wakuu katika kuongeza upatikanaji wa nishati vijijini hawawakilishwi katika wakala hiyo kwa vile mwakilishi wa sekta binafsi anatoka katika jumuiya ya watumiaji,” alisema Matimbwi.

Katika hafla hiyo yenye kaulimbiu ya mwaka 2024: ‘Nishati Mbadala kwa Uchumi Shirikishi na Kijani,' mgeni rasmi aliwashukuru wafadhili wa tukio hilo wakiongozwa na Sunking kama mfadhili mkuu; Wizara ya Nishati; Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP); Utaalamu Ufaransa, TANESCO, Ensol Tanzania Limited, Global Off- Grid Lighting Association (GOGLA); Africa Enterprise Challenge Fund (AECF) na Umoja wa Ulaya (EU).

Kwa mujibu wa Luoga, kwa kutambua uwezo katika kuhakikisha ugavi wa uhakika na upatikanaji wa nishati ya kisasa kwa wote ifikapo mwaka 2030, serikali inajiandaa kuzindua Mkakati na Mpango Kazi wa Kitaifa wa Nishati Jadidifu utakaochochea uwekezaji mkubwa katika nishati jadidifu jambo litakaloakisi vyema Dira ya Tanzania ya 2026; Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2015; na makubaliano mengine za kimataifa na kitaifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

“Hata hivyo, Serikali inaandaa “Mkakati na Mpango Kazi wa Ufanisi wa Nishati Tanzania” utakaosaidia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Nishati na malengo ya kimkakati ya kupunguza kasi ya nishati kwa asilimia 20 ifikapo mwaka 2025. Lengo la jumla ni kuhakikisha upatikanaji wa huduma za gharama nafuu na za uhakika za nishati endelevu na ya kisasa kwa wote wananchi wote,” alisema.

"Kwa kuhama kutoka kwenye matumizi ya mimea asilia kama vile kuni na mkaa kwa kupikia, hatupunguzi hewa chafu tu bali pia tunaboresha hali ya hewa na kuboresha maisha ya mamilioni ya watu katika maisha yajayo Utekelezaji wa mkakati huu unasaidia moja kwa moja Msaada wa Kupika Safi kwa Wanawake wa Kiafrika..

“Mpango huu unalenga kuwawezesha wanawake barani Afrika kupitia warsha za ujasiriamali kuhusu upishi safi; kuanzisha kongamano la pamoja la nchi za Afrika kuhusu kubadilishana uzoefu; kuongeza viti vya wanawake kwenye nafasi za usimamizi; kuinua usawa wa kijinsia na kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi duniani kwa ujumla,” alisema.

Kamishina wa Umeme na Nishati Jadidifu Tanzania, Mhandisi Innocent Luoga akiwa katika Banda la d.light ambao ni moja ya washiriki wa Maadhimisho ya Wiki ya Nishati Jadidifu  (REW) Mwaka 2024. 

Baadhi ya washiriki wa Maadhimisho ya Wiki ya Nishati Jadidifu  (REW) Mwaka 2024 wakijisajili kwenye maadhimisho hayo. 

Wadau wanaotembelea maonesho wakiwa katika Banda la d.light ambao ni moja ya washiriki wa Maadhimisho ya Wiki ya Nishati Jadidifu  (REW) Mwaka 2024.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad