HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 15, 2024

Sahara Ventures yaitangaza rasmi Sahara Sparks 2024

 

Sahara Ventures imetangaza rasmi tukio la Sahara Sparks 2024 litakalo fanyika tarehe 27 na 28 Septemba katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, Tanzania.

Sahara Sparks ni jukwaa linalo waleta pamoja wabunifu mbalimbali wa teknolojia, wafanyabiashara pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo na teknolojia na kuwapa fursa ya kushiriki maonesho ya kibiashara pamoja na kujadili maswala mbalimbali ya teknolojia, maendeleo na uchumi. 

Kwa takribani miaka 9 sasa Sahara Sparks imekua ikifanyika kila mwaka na kwa mwaka huu inakuja na kaulimbiu ya “Watu, Ujuzi na Ulimwengu mpya wa ajira”.  

Kwa kutambua changamoto na pengo lililopo baina ya ujuzi unaohitajika na ule unaopatikana katika soko la ajira, Sahara Sparks inalenga kukabiliana na changamoto hii kwa kuandaa mijadala mbalimbali itakayo ongeza ufahamu kuhusu hii changamoto na kuleta suluhu za kimkakati ikiwemo kuunda sera zitakazo saidia kutatua changamoto hii.

Akizungumza na vyombo vya habari wakati wa kuitangaza rasmi Sahara Sparks katika ofisi za Sahara Ventures Mhandisi Samson Mwela , Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ali toa rai kwa  kampuni changa za ubunifu wa teknolojia (startups), sekta binafsi na wadau mbalimbali wa maendeleo kushiriki kwenye maonesho na mijadala mbalimbali itakayo andaliwa katika wiki ya Sahara Sparks ambayo kilele chake kitakua tarehe 27-28 Septemba, 2024 kwenye ukumbi wa Mlimani city.

“Wiki ya Sahara Sparks imeandaliwa kwaa ajili yetu kwahiyo wote tushiriki hususani kampuni changa za ubunifu wa teknolojia zinazo fahamika kama Startups, sekta binafsi na wadau mbalimbali tutumie fursa hii kama njia ya kutangaza biashara zetu kwa kupitia maonesho yatakayo fanyika mlimani city mwezi Septemba mwaka huu, pia tushiriki mijadala ili kwa pamoja tutatue changamoto za ujuzi na ajira” alisema.

 Mhandisi MwelaMkurugenzi mtendaji wa Sahara Ventures Bw. Jumanne Mtambalike sambamba nakuhamasisha ushiriki wa wadau mbalimbali alielezea umuhimu wa mijadala itakayo fanyika katika wiki ya Sahara Sparks 2024.

“Mwaka huu tutaandaa mijadala mbalimbali itakayo anagazia namna gani teknolojia, ubunifu na ujasiliamali unavyosaidia kuongeza ajira na kukuza uchumi wa taifa. Majadiliano haya yatatilia mkazo zaidi kuhusu rasilimali watu hususani vijana na jinsi ya kuwaandaa kwaajili ya ulimwengu mpya wa ajira.” alisisitiza Bw. Mtambalike.

Sahara Ventures inakaribisha sekta binafsi, startups, washirika wa maendeleo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, watunga sera, wataalamu wa uvumbuzi na teknolojia, wajasiriamali na wadau wengine kushiriki tukio hili la kihistoria. 

Kwa taarifa zaidi ya jinsi ya kushiriki au kudhamini tembelea tovuti ya www.saharasparks.com  
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad