HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 4, 2024

NSSF YATUMIA MAONYESHO YA 11 YA BIASHARA NA UTALII KUITANGAZA NSSF TAARIFA


MKUU wa wilaya ya Muheza Zainab Abdallah akizungumza mara baada ya kutembelea Banda la NSSF mapema leo wakati wa maonyesho hayo 

Mkuu wa wilaya ya Muheza Zainabu Abdallah kushoto akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mkuu wa Matekelezo Mkoa wa Tanga Wa MFUKO wa Taifa wa Hifadhi za Jamii nchini (NSSF) Abubakari Soud Mshangama

MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian kulia akisalimiana na Afisa Matekelezo Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga Abubakari Soud Mshangama wakati alipofika viwanja vya shule ya Sekondari Usagara kufungua Maonyesho ya 11 ya Biashara na Utalii

MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batild Burian kulia akipata maelezo kutoka kwa Afisa Matekelezo Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga Abukabari Soud Mshangama














Na Oscar Assenga,Tanga


MFUKO wa Taifa wa Hifadhi za Jamii nchini (NSSF) wameshiriki maonyesho ya 11 hya Biashara na Utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara Jijini Tanga huku wakiitangaza huduma yao mpya ya NSSF Taarifa.


Akizungumza leo Afisa Matekelezo Mkuu wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakari Soud Mshangama ambapo alisema mpango huo ni muhimu kwa sababu unamuwezesha mwanachama kupata taarifa binafsi ,michango na madai yake.


Alisema huduma hiyo inapatikana kupitia simu ya kiganjani kwa njia tatu ambazo ni ujumbe mfupi (SMS),Programu ya simu ya Kiganjani (Mobile App) ya NSSF na WhatApp.


“Leo tupo hapa kwenye maonyesho haya pamoja na kutoa elimu kuhusu huduma zetu lakini pia tunatumia kuitangaza Programu hii inamuwezesha mwanachama kupata taarifa na huduma mbalimbali kwa njia ya ujumbe mfupi”Alisema


Aidha alisema pia walikuwa wakieleza mafao yanayotolewa na Mfuko huo na vigezo vyake ikiwemo Mafao ya Pensheni ya Uzeeni ambayo mwanachama hulipwa kila mwezi kwa anayetimiza vigezo vilivyowekwa.


Awali akizungumza mara baada ya kutembelea Banda la NSSF Mkuu wa wilaya ya Muheza Zainab Abdallah alisema NSSF ni muhimu sana huku akiendelea kuwataka wafanyakazi na wasiowafanyakazi kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na mafao mbalimbali ikiwemo ya matibabu,dharura kama wamepata magonjwa hivyo wanapoweka akiba yako ikitokea umepata jambo lolote ni rahisi kukuhudumia.


Alisema wanapoweka akiba yako inakuwa ni rahisi unapokumbana na changamoto mbalimbali inakuwa ni rahisi kuweza kukuhudumia na kukupa matibabu ikiwemo unapofikia umri wa kustaafu unaweza kuwa na akiba yako ambayo inaweza kukulea mwenyewe.


“Niendelee kuwahimiza wafanyakazi na waajiri wajue kwamba ni takwa la kisheria wahakikisha wanawaingiza watumishi kwenye mfuko wa hifadhi za Jamii (NSSF) ili kuweza kunufaika na huduma mbalimbali ”Alisema

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad