HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 24, 2024

NAIBU WAZIRI RIDHIWANI KIKWETE ATEMBELEA BANDA LA TIB MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete ametembelea Banda la Benki ya Maendeleo TIB katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.

Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yalianza rasmi tarehe 16 Juni, 2024 na yanatarjiwa kukamilika tarehe 23 Juni, 2024.

Kaulimbiu ya Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2024 ni: Kuwezesha kwa Utumishi wa Umma Uliojikita kwa Umma wa Afrika ya Karne ya 21 Iliyojumuishi na Inayostawi; Ni Safari ya Mafunzo na Mabadiliko ya Kiteknolojia.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akipokea zawadi kutoka kwa Meneja Uhusiano na Masoko wa Benki ya Maendeleo TIB mara baada ya kutembelea banda la TIB wakati Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea Banda la Benki ya Maendeleo TIB katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Benki ya Maendeleo TIB wanaoshiriki Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akiagana na watumishi wa Benki ya Maendeleo TIB mara baada ya kutembelea banda la TIB.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad