HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 8, 2024

KAMPUNI YA UENDELEZAJI JOTOARIDHI TANZANIA YAANIKA MIPANGO YAKE,YATAJA MIRADI

 

 

Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV 


KAMPUNI ya Uendelezaji Jotoaridhi Tanzania (TGDC) ambayo ni Kampuni tanzu ya Tanesco imesema inaendelea na mkakati wake wa kuchoronga visima vya nishati ya jotoaridhi kwa lengo la kuhakikisha inatumiwa katika vyanzo vingine kama umeme.


 Akizungumza katika Kongamano lililowakutanisha wadau mbalimbali ambao wanatumia vyanzo vya nishati vinavyotokana na jua ,upepo na jotoaridhi,Meneja Mkuu wa wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoaridhi Tanzania (TGDC) Mhandisi Mathew Mwangomba ameeleza mikakati mbalimbali wanaoendelea nayo katika kufanikisha nishati ya jotoaridhi inatumika nchini.

" Tumenuia lazima kwanza tupate nishati safi ya jotoaridhi ambayo Tanzania kwa maana ya uendelezaji wa jotoaridhi Tanzania Ina maeneo matatu ya kipaumbele .Eneo letu la kwanza liko Ngozi katika Mkoa wa Mbeya na kwa sasa hivi tuko katika hatua ya kuhakiki rasilimali ya jotoaridhi Tanzania 

"Sasa tutakapoipata hii nishati safi kwa maana jotoaridhi,tutakuwa na vyanzo vingi vya umeme,tunatambua umeme ni biashara,uchumi,afya, sanaa na umeme ni michezo. Kwa hiyo sisi Kampuni ya Uendelezaji jotoaridhi Tanzania tumekusudia kuhakikisha hii nishati inatumika...

"Na kama vile ilivyokuwa kusudio la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha kwamba nishati safi inatumika na inamuendeleza Mtanzania. Sasa katika matumizi hayo tunaweza kutumia matumizi ya moja kwa moja, joto hili ambalo tunalivuna kutoka katikati ya Dunia kuja katika tabaka la Dunia,"amesema .

Ameongeza nishati hiyo ya jotoaridhi inaweza kutumika  kwa kupikia ,kwa Kilimo,utalii na mambo mengine pamoja na kuvuna madini muhimu huku akifafanua Dunia sasa hivi inakwenda katika kuwa na nishati safi kwa maana ya kuwa na magari ya umeme na gesi.

Mhandisi Mathew anasema Tanzania imepitiwa na  bonde la Ufa katika maeneo mengi  yana rasilimali ya nishati ya jotoaridhi akitolea mfano eneo la Kejo mkoani Mbeya, Songwe pamoja na Nguruwi lakini na upande wa pili wa nchi ya Kenya nao wana nishati hiyo ya jotoaridhi.

Amesema dhima yao ni kuhakikisha wanapata nishati safi,na kwamba kuna rasilimali ya megawati 5000 kwa sasa hivi ya nishati safi kwa maana ya umeme na megawati 5000 kwa nishati ya moja kwa moja.
Awali Afisa Mkuu wa Mawasiliano Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) Khadija Ahmed
 Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC)...amesema jotoaridhi ni nishati safi salama na rafiki wa mazingira na ni nishati ambayo haithiriwi na mabadiliko ya tabianchi .

Amefafanua nishati ya jotoaridhi ni nishati safi, salama na rafiki wa mazingira,huwa haithiriwi na mabadiliko ya tabianchi iwe masika,kiangazi na wakati wote inapatika tofauti na nishati ya umeme unatokana na maji ambapo Kuna wakati mabwawa yanajaa maji mengi wakati wa kiangazi na maji yanakauka wakati wa kiangazi.

"Nishati ya jotoaridhi mnapoanza tu kuichimba basi mtachimba mpaka mwisho wa Dunia, inaendelea kutumika labda kitakachokuwa kinafanyika ni matengenezo madogo madogo ambayo hayawi makubwa ukilinganisha a nishati nyingine ambayo inazalishwa nchini kwetu.

"Tanzania  tumebarikiwa jotoaridhi kwani  inapatikana katika mikoa 16 na katika hiyo mikoa kuna sehemu 52.Tumepita katika maeneo hayo,tumeipata nishati ya jotoaridhi kwa hiyo tunaenda na hatua mbalimbali muhimu 
"Kwasababu  nishati yoyote tunasema ni mchakato,sio kitu cha kupata mara moja ,kwa hiyo kwasasa hivi Kampuni yetu tunashukuru Serikali yetu kupitia Wizara yetu ya nishati na Kampuni mama yetu Tanesco tumeweza kufanya utafiti ambao tumefikia hatua ya kuhakiki visima vya jotoaridhi ambapo tuna Miradi minne.

"Katika miradi hiyo tunategemea kuanza kuzalisha nishati yetu ya jotoaridhi ambayo kwa sasa mtambo wetu wa kuchoronga visima vya jotoaridhi tayari uko mkoani Mbeya,tunategemea kupata megawati 70"amesema.

Ameongeza kuwa kwa sasa hivi wako katika hatua za kukamilisha taratibu za manunuzi kwahiyo wakati wowote kuanzia sasa wanaweza kuanza kuchoronga visima katika mradi wao  wa Jotoaridhi Ngozi ambapo mitambo ya kuchoronga iko kazini.

Kuhusu kongamano hilo imeelezwa  limekutanisha wadau mbalimbali ambao wanatumia vyanzo vya nishati vinavyotokana na jua ,upepo, jotoaridhi lakini matumizi ya nishati safi ya kupikia kama ambavyo tumeona 

Pia kongamano hilo linakwenda sambamba na juhudi za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ambaye mwezi uliopita amezindua mkakati wa kitaifa wa miaka 10 wa matumizi ya nishati safi ya kupikia na kwamba mkakati huo unalenga kuhama kutoka kwenye nishati isiyo safi kwenda kwenye nishati safi.

Kwa mujibu wa Rais Samia lengo ni kuona asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2024 mpaka 2034.



 



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad